Ubunge wa viti maalumu kutoka cdm utakuwa na maana sana kwa ccm endapo hao wamama watakuwa wanachama hai wa cdm, vinginevyo inakuwa ni biashara ambayo hailipi kwa ccm,
ccm aka gambas wanawahitaji hao wamama wa cdm ili justify kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki hivyo kuwafanya Serikali kupata msaada sasa kitendo cha cdm kuwafuta uwanachama kimeharibu kila kitu,
na hii ndio sababu imewafanya kuwataka hao wamama wajirudi na kureconcile na chama chao ili lengo lao litimie, ila kiufupi hili bunge kama akina halima kipindi kile walikuwa wanapewa adhabu ya kukaa mwaka nje ya bunge, this time watapewa adhabu ya kuwa nje ya bunge kwa vipindi vyote au kuwavua kabisa huo ubunge as long wao wanapata mpunga toka kwa wahisani.
Sasa sijui kwanini akina halima hawalioni hili, kwamba wao wanatumika tu kama rubber stamp, baada hapo wanatupwa huko, Kifupi hao wamama wakae pembeni maana naona wamelewa madaraka kiasi cha kujiona wao ni untouchable.