CCM haipo hivyo tena. Haiangalii utawala wa sheria. Kwa kuwa hawana tena ridhaa ya walio wengi hutumia hoja ya nguvu na ubabe. Walipora kwa nguvu uchaguzi wa vijiji na serikali za mitaa. Haiwezekani kwa levo ya upinzani ilipofikia CCM wapate asilimia 100 ya mitaa na vijiji vyote. Uharamia ulitumika. Wamepora uchaguzi wa madiwani, wabunge na raisi.
Huenda wangelishinda lakini sio kwa asilimia 100. Uharamia na ubabe ulitumika kupora ushindi kwa aslimia zote hizo. Kwanza Ndugai anaona aibu kuwa waliiba ushindi kijinga. Sasa kuna bunge la chama kimoja. Fomula ya kupanga Kamati za bunge inatatizika kwa kuwa kikanuni kamati zingine lazima zisimamiwe na wapinzani.
Anatumia nguvu nyingi na ubabe uleule kupata wapinzani ndani ya bunge. Hiyo hapo ni njama yake na Mahera wa NEC kuwarubuni akina Mdee ili kujaribu kuficha aibu ya uso.