Wengi humu naona zaidi tumekuwa wa kushabikia kuliko kusaidia, Haijulikani kama wapo wanaotaka kuendelea kumuona Jide jukwaani ama la, Kama muwashabiki wa Jide nini ushauri wenu kwake ili aweze kuendelea kuchanua ?
Kwa upande wake Jide anaweza kuwa anafurahia wanaomuunga mkono kwa michango yao lakini akumbuke binadamu sie ni vinyonga, Ni hao hao ambao humu wanakushabikia ndio hao hao ambao hawatokuwa na habari na wewe pindi utakapopotea kimuziki, Refer kwa kina SAIDA na wengineo..
Kwa kitendo cha Jide kutamani kushirikiana na wasanii wa THT ni ushahidi tosha kuwa anakubali na kuiona thamani ya wasanii hawa, Ni ubishi wa kujilazimisha tu ndio utapinga hili. Sasa swali langu kwenu pamoja na dada Jide..Thamani hii inakuja hivi hivi au inaundwa ? Nawe Jide si umekuwa na jina kubwa kwa sababu uliundwa ? Sasa hiyo THT ni nini ? (sihitaji kujibu hili majibu wote mnayo)....Kinachoelea kimeundwa..Najua wachangiaji humu "tumejaaliwa" hivyo tuwagumu kuona hili.
Ushauri wangu wa Jide ni kwamba bado una nafasi ya kutengeneza mambo, Bifu zisizo na maana hazikujengi bali zitakubomoa. Wewe ni mwanamuziki na kipaji unacho..Wakati mwingine mambo sio rahisi kama unavyofikiri. tafuta ushauri..ongeza ubunifu..Walikupokea vizuri wanainchi na bado nafasi ipo iwapo tu utawapa wanachotaka. Support na ushauri uliowahi kupata nadhani bado unahitajika usidanganywe na watu wachache. Una mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzako kama DULLY SYSKES, Bado tunamsikia sio kwa sababu tu aliwahi kuwika siku za nyuma, Bali ni kwa sababu anajitahidi kwenda na wakati (kusoma alama za nyakati). Usifikiri wewe ni special sana kuliko wale ambao leo hii wamepotea mfano Mr Nice, Saida Karoli na wenginewe..Kipaji hakizuiliki...na wala kutofautiana na clouds hakutokuletea tija yoyote. Sanasana kuna mambo yatakukwamisha. Ona kwa mfano umeshindwa kushirikiana na wasanii wa THT kwa sababu tu umetofautiana na menejimenti inayowasimamia...hapa nani amepoteza ? Na kila binadamu ukimpa kalamu na karatasi aandike matatizo yake kitabu kitajaa. Haya yote yataisha iwapo tu utaongeza bidii kwa kile ambacho umejaaliwa, nacho ni kipaji cha MUZIKI. Huna sababu yoyote yakutofautiana na clouds.
Na wale ambao wanaona Ruge anawanyoya wasanii, Swali langu kwao ni hili. Hivi huyo ruge ni taasisi inayojitolea ? Kama ameamua kuwekeza kwenye muziki si lazima awe na makubaliano yatakayomuwezesha yeye na hao wanamuziki wanaendelea kuwepo ? Au tunatamani tuone wasanii wakifanya shows kila kukicha, kupata mikataba tofauti tofauti naye Ruge abaki kama mshika pembe. Then what ? Si tungeishia kumdharau kama tulivyozoea kuzarau wale waliokosa mipango ? Mlitaka abaki kule kwenye smooth vibes huku Jide akiendesha prado ? Then nani angeonekana -----...Kama Jide aliona ananyonywa ni nini tunasema kuhusu kina marehemu Marijani ? Nani asiyejua mchango wa marehemu Marijani Rajabu na maisha aliyokuwa anaishi ? alinufaika vipi na kazi zake, Au naye alihitaji "wanyonyaji kama Ruge ili anufaike ? Ni kipi tunachotaka kuona kwa Jide ili tuone ya kuwa alifaidika na jasho lake ? Tuache kuendeshwa na hisia za kudhani kwamba Jide alistahili kuendesha ndege na sio prado ili tukubali kuwa alifaidi jasho lake ?