Nimemuona Hassan Mwakinyo akipigana, maoni yangu ni haya

Nilifurahia mpambano wa wale wadada, mmoja wa kenya na mwingine wa Zambia. Mwakinyo sikufurahia pambano lake, sikulielewa, nadhani nikiangalia pambano linguine ndo nita m judge
 
mwakinyo ana uwezo wa kumpiga antony joshua
Hapa kwa uandikaji wa siku hizi, wachache utaelewana nao. Una maana "ana uwezo" katika maana ya "he is able" au "hana uwezo" katika maana "he is unable"???? Kwa sababu hiyo "h" kukosekana au kuwepo, inaleta maana mbili tofauti kabisa. Please clarify, ni "ana" au "hana"???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna pambano moja la mwakinyo alimpiga mzungu kwa KO, alichotumia ni kushambulia kwa kurusha ngumi nyingi mfululizo hadi mzungu akalemewa. Nadhani siyo technique nzuri sana ukikutana na bondia mwenye physique nzuri na ngumi nzito, kwa sababu unaporusha ngumi nyingi sana ambazo hazilengi target unakosa concentration katika kujilinda na possibly unaweza kuchoka mapema
 
Mkuu ni TKO fuatilia pambano uone.
TKO ni ile bondia anakula ngumi hadi refa anamuonea huruma kwamba atakufa huyu, TKO bondia ahesabiwi ile 1 hadi 10.

Ila KO ni kwamba bondia anakula ngumi anakwenda chini, anahesabiwa hadi kumi, asiporudi ground hiyo ndio KO brother. Nijuavyo mimi lkn ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao kina Dulla Mbabe ndo hamna kitu kabisa, wanapigana kama ameatur, rejea pambano lake na Cheka. Mwakinyo kidogo anaonesha utofauti, japo ana tatizo la defence, akirekebisha hilo atafika mbali maana kurusha ngumi kali anaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akikutana na mtu wa jamii ya Mayweather atachoka mapema, maana akirusha ngumi zake 20 zinaweza kumpata mbili tu tena dhaifu kwa jinsi jamaa anavyojua kukwepa, matokeo yake atachoka mapema na kupigwa kirahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Hili tatizo analo tangu pambano na sam, ingawa ameimprove kidogo, lakini swala la ulinzi inabidi alifanyie kazi...... maana kuna mijitu ina technik za kudokoa sura balaa....... asipolewa sifa, atafika mbali kwa kuwa ana ngumi zinazoumiza
 
Mwakinyo ngumi zake utasema anasomea Youtube, ukweli kinachomrudisha nyuma sasa hivi ni kocha mzuri tu, uwezo anao na nia ya kua bora anayo, kinachomuangusha kupata kocha anayeelewa ngumi vizuri ka bongo ni kazi sana. Na jamaa life bado halijamyookea kivile, akijua technique vizuri anaweza fika mbali.
 

Kama kweli unazijua ngumi sidhani kama unaweza kumsifia Mwakinyo kwa mapambano mawili aliyopigana ambayo yote hayakuwa ya ubingwa wowote zaidi ya kuwa mapambano ya utangulizi, pambano la juzi Nairobi amepigana na Muargentina mwenye miaka 41 na anaonekana kabisa yuko dhaifu..

Binafsi mapambano mawili ya namna ile huwezi kuniambia jamaa ni good boxer kiasi ya kumpa sifa tunazompa.. Rashidi Matumla, Mbwana Matumla walipambana mapambo mengi ya ubingwa walileta mikanda hivyo walistahili sifa kubwa...

Mwakinyo apambane na mabondia baadhi wa nyumbani ili adhihirishe ni bondia bora Tanzania, huwezi kusema ni bondia bora Tanzania wakati hakuna hata bondia mmoja wa ndani aliye bora ambaye umempiga zaidi kushinda mapambano ya utangulizi mawili..

Rashidi Snake boy kila mtu anamjua alivyowakarisha akina Maneno mtambo wa gongo, Cheka nk, Mbwana pia anajulikana alivyowakarisha mabondia wengi wa ndani kiasi cha kufikia namba tatu duniani WBC kwenye uzito wake..

Mwakinyo anapewa Umaarufu ambao hastahili kwenye boxing lakini bondia wa kawaida sana sana.. na tukiendelea kumpa kichwa hivi tutampoteza AFANYE MAZOEZI APIGANE MAPAMBANO MENGI YA UBINGWA NA YANAYOTAMBULIKA NA VYAMA VYA NGUMI, WBC, WBA, IBF nk kama wenzie maarufu waliomtangulia..
 
Kijana anajitahidi sio wale wanaenda kuuza pambano..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…