Joseph lebai
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 8,452
- 8,670
Mara nyingi ndoto ni kinyume chake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi tena chakeNdugu wana jamvi kwanza nikubali kwamba nimechelewa kuhadithia ndoto yangu maana muda huu umeendelea sana. Lakini sio mbaya nikasimulia kile nilichoota usiku wa kuamkia leo.
Baada ya kupata chakula cha usiku nimepumzika kidogo huku nikisubiria mechi ya Arsenal na Liverpool iliyoanza saa nne usiku. Baada ya mechi hiyo ambayo kimsingi imetoa matokeo mzuri kwa team yangu pendwa, nilienda kulala.
Hii ndio ndoto yangu; watu walikuwa wameshika matawi ya miti na wengine wakiwa na vuvzella walikuwa wanashangilia ushindi wa ubunge. Kulikuwa na vijana wengi wanaimba GWAJI!! kwa kurudia rudia katika mpangilio mzuri. Baada ya muda mfupi nikamuona Askofu Gwajima ametoka nje huku anatabasamu na kuwashukuru wananchi wote kwa ushindi.
KISHA NIKAAMKA USINGIZINI.