Mzee mengine nimeona niyaache kwanza ila hili nitalijibu hapa ingawa si mahala pake, kwa bahati mbaya hapa hatujuani kwa majina ila niamini ninapokuambia nimepata bahati ya kuishi sehemu nyingi duniani kwa vipindi tofauti tofauti, nimeishi karibu mabara yote ya dunia tena nikiwa na bahati ya kushuhudia mabadiliko makubwa makubwa makubwa.
Nimeishi wakati sheria za ubaguzi zinaishia ishia Marekani, nimeishi wakati Russia ikiwa ni taifa kubwa, nimeishi ujerumani wakati ukuta wa Berlin ukianguka na pia nilikuwa Rwanda wakati Genocide inalipuka, nime save Bosnia kama askari wa kulinda amani na nilikuwa volunteer wa uchaguzi juzi wakati Bingu wa Mutharika wa Malawi aningia madarakani kwa matumaini makubwa.
Niamini ninapokuambia hakuna system iliyokamilika duniani na hakuna mwenye suluhisho la matatizo yoote ya mwanadamu in one package, so misimamo yangu ya kisiasa haina uhusiano kabisa na suluhu ya maisha bora kwa kila mtu. Siamini na sitegemei kuona jamii inayoishi kama peponi, kwa bahati mbaya sana pia mimi ni mjamaa hivyo naamini katika misuguano katika jamii na matabaka yanayo sababishwa na ukomo wa resources.
Nitampinga na kumdharau kila mwanasiasa anayewahadaa watu kuwa yeye ni mtume mwenye suluhu ya matatizo ya watu. Hii ni falsa yangu na ndio inayoniongoza katika misimamo yangu yangu.