Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika Taasisi ya Serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja.
Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulibadilishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula.
Semina iliisha Ijumaa na tuliagwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.
Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi nina miaka mingapi?
Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alishtuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka.
Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je nina mtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye ana miaka 31, anakazi nzuri sana.
Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwa sababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake.
Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza ana miaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao.
Ushauri jamani