Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika Taasisi ya Serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja.

Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulibadilishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula.

Semina iliisha Ijumaa na tuliagwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi nina miaka mingapi?

Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alishtuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka.

Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je nina mtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye ana miaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwa sababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake.

Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza ana miaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao.

Ushauri jamani

hiyo uliyo pata ni bahati sana
itumie vyema zaa na huyo kijana ila hata mkiachana ubaki na ukumbusho na uitwe mama
coz umri nao unazidi kuyoyoma,
pili ukikutana na mzee wa umri wako au aliye kuzidi umri atakuzeekea tuu bora kijana akupe shughuli ya haja.
anywey akili kumkichwa but umri sio shida sana na kijana kaamuwa kuwa wazi kwako
 
44yrs , no Husband no kid/kids...Nadhani its too late...honestly.. ukizaa now..ukifika 50 yrs mwanao ndo atakua 6yrs..yani hata shule hajaanza,.

Its too late. lets be realistic .
 
Dada mpaka sa8 usiku mnaongea tuu live bila chenga wala umeme kukatikakatika??
ushauri....wewe kama mnapendana bebaneni tu muoane tena kwa shangwe zote! wambie unamiaka28! kwani wakwe watadai cheti cha kuzaliwa???
Lol bebaneni,love is love sex is sex
 
Kuna wakati wanaume tuwe tunaangalia mbali na si mbele tunapofanya analysis ya mambo ambayo yana umuhimu sana maishani.
Tofauti ya miaka 12 kweli?!
 
Sky Eclat bado hujafikia uamuzi tu? ni toka mwaka jana (2015) ujue....🙂🙄
 
Kipendacho roho,hula nyama mbichi. Fanyeni yenu.
 
A true LOVE has no reason, but accompanied by endless and unconditional sacrifices and commitments....! And a real and everlasting marriage do come alone with no sake....! With exception of telling your LORD what you need, do not struggle to seek marriage, let it come automatically....!
 
Mmmh, huyo kijana ni limbukeni sana. Yaani wewe tafuta mzee mwenzio. Huo utakuwa ni wizi wa mapenzi hata wazazi wake na jamii watakushangaa.
 
Miaka 44 hujafika tu menopause kama bado basi uko kwa pre-menopause sooooo bila kufikiri sana kuhusu possibility ya kuolewa ukapoteza muda ukajikuta umefika kikomo zaanae tu jamaaa na huenda ikawa pia kigezo cha mizengwe inayohofiwa toka kwao na jamaaa
 
Umezaliwa 1967 halafu dogo wa 1985
kama umempenda poa mfunge ndoa tu .
 
hivi mwanmke wa miaka
Usithubutu kuzaa, huu ushauri wa bure tu nakupa!
Kwani wangapi wamezaa na wameachwa?.

Km kweli yupo serious na ni mpango wa Mungu itakua tu dada yangu!!...

Huyo Dada ako nae ataingiliaje mapenzi ,hajui ni makubaliano ya watu 2!
.sorry,huyo Dada ako kaolewa?

Huyo kaka anasema kwao wataleta zengwe,kwahiyo ataenda kuwatangazia ndugu zake kuwa umemzidi?..
If so,hayupo tayari kukudefend huko kwao!?

Dada Yangu muombe Mungu,ukipata amani moyoni jua ndie ,na km ndie hakutakuwa na chochote kitakachozuia,means kila mmoja wenu atakua tayari kudefen penzi lenu!!

Nb:naona anataka kujua km unaweza kuzaa.
Mtazamo wangu tu!!!
44 bado anazaa...hata hivyo kama anazaa bora azae tu coz kwa mwanamke miaka yote hyo then mnamshauli asizae...it is not fair....otherwise kama ameamua au hana haja na familia..
 
Kuna wakati wanaume tuwe tunaangalia mbali na si mbele tunapofanya analysis ya mambo ambayo yana umuhimu sana maishani.
Tofauti ya miaka 12 kweli?!
Uko sahihi mkuu
Hata Nick Canon alimkimbia Mariah Carey
 
Back
Top Bottom