Nimemzuia mke wangu kupanda lift ya jirani, lakini amekaidi


Hahahahahhahahaha! Hahahahahhahahahaha! Dah umenichekesha sana. Eti anaringa sana na kigari chake. Sasa mkuu fanya hivi. Wewe panda daladala, kasha mwachie waifu gari awe anaenda nayo kazini. Wakati unajipanga kununu gari linguine. Utakuwa umeepusha hii shari.
 
Suluhisho linguine ni kumwambia huyo muasherati ni marufuku kumpa lifti mkeo, hata kama akimkuta ananyeshewa na mvua. Hiyo itamfanya aogope. La sivyo kuna hatari kubwa ya kumegewa, mkakosa amani kwenye ndoa. Na amani ikikosekana kwenye ndoa, mambo huenda mrama sana. Kuliko hata unavyofikiria. Yaani wanasema, usidharau matatizo madogo madogo katika maisha, kwani tundu dogo tu linaweza kuzamisha meli nzima.
 
Hapo kwenye red du! Muwindaji huyo.
Changamoto mwanawane. Naungana na walioshauri umwachie mamaa mkoko. Wewe kula guu mpaka utakapojikusanya na kumnunulia mamaa la kwake. Kizazi hiki ni shiiiida!
 
kikubwa si wanapakia wengi mkuu,angekuwa anapakia mwenyewe hapo ndio shida
 
mwachie gari wewe ukomae na public transport .......... pia si kila mwanamke ni maharagwe ya Mbeya ondoeni hizo fikra kichwani mwenu
 
Haaaa haaaa hilo lijamaaa ni shida lazima atammega mkeo hakuna jinsi we tulia tu.
 
You are a man..Nakubaliana na juhudi unazofanya kulinda ndoa yako..makazie huyo kama vp kampige mkwara jamaa asimzoee mkeo maana atakuletea aibu kwny ndoa yako..
Wanaume wa ******* sana jamaa akimzingua huyo mwingine lazma aje alipize kisasi kwa kummega mke wa jamaa ili kumwonesha kweli yy ni kidume!! jamaa kama mjanja mbadilishe ratiba amwahishe mke kazini halafu yy aendelee na mishe zake au amwachie mke gari kumpiga mke siyo kuluhisho
 
Ukiweza kuishi na mwanamke katika nyakati hizi ngumu.......basi una uwezo hata wa kuishi jahanamu bila shida yoyote....maana kuishi na kiumbe wa kike katika kipindi hiki kunahitaji kipaji cha uvumilivu....
 
kikubwa si wanapakia wengi mkuu,angekuwa anapakia mwenyewe hapo ndio shida

Hao wengine ni singles. Plus, kwa kifupi, haingiii akilini mkeo kupanda gari la mtu ambaye wewe huwa hata hakusalimii, achilia mbali gari la rafiki yako. Wanawake huwa wanavutiwa na mazungumzo, sio mwonekano wa mwanaume. Sasa akipata wasaa wa kukaa nae kwenye foleni masaa mawili, usishangae yatayotekea.

Juzi tu hapa hapa JF, kwenye jukwaa hili kuna mwanamke, tena mke wa mtu, amekiri kwamba anavutia na kichaa wa mtaani kwao ambaye huwa anatembea akiwa mtupu! Na kichaa ana limashine la kutosha! Ni bure kuepusha shari!
 
Mkuu, minasubiri mrejesho ukija kuskia karudia kupanda lifti ya hilo Li jirani[emoji12]
 
Mnunulie ndipo umuzuie kupanda ya wengine
 
Acha nijikusanye sanye, hali ikieleweka nitafanya hivyo mkuu
hakuna jambo linalouma kama kumegewa wife wako aisee usiombe ikakutokea unaweza kuua mtu bila kusudio pole sana mwelekeze mkeo aachane na mpango huo yy apande usafiri wa kawaida kama nyumbani bado hamjapata usafiri wenu avumilie kipindi hiki kifupi asije akakukasirisha zaidi
 
MKEO HAKUHESHIMU/SIKILIZI.
WHICH MEANS ..................
 
Madai yako una usafiri kwanini sasa unamuacha wife home wakati nae anaenda kazini?
 
Lakini umesema jirani alikua anakupita kituoni pindi huna gari, means we na jiran mnafanya kaz uelekeo mmoja? Sasa yy ampeleke wife wako anampaje lift. Pili usafir qa dar n mgumu sio km siye huku mikoan toyo ya buku tu unawai kazin. Kuzuia mkeo asipate majaribu ondoka nae hata kama n SAA kumi na moja na km hataki Kuwai bas apande daladala
 
Hilo gari lako mpe wife aende nalo kazini then wewe panda daladala. ili usipate tabu ya kuukondesha moyo kwa wivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…