Nimenunua bodaboda aina ya Sinoray 250 ADV. Nawezaje kuifanya kuwa stable?

Ni Mateso tu.

Mafuta kubugia sana

Spoku za nyuma kukatika... Ndio nimebadilisha na kuweka sport rim!! Za bila spoku japo Zika gharama sana.
 
Asante kwa mrejesho,utawasaidia wengine katika kufanya maamuzi/machaguzi
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Ni Mateso tu.

Mafuta kubugia sana

Spoku za nyuma kukatika... Ndio nimebadilisha na kuweka sport rim!! Za bila spoku japo Zika gharama sana.
Pole sana.kweli hapo mchina wa sinoray amezingua pakubwa.nina XL125 ya urithi ina kama miaka 30 naa ila hadi leo naitembelea spoko zina kutu ila rimu ipo stable na hazichomoki!mazingira iliyopo haijui lami ni nini kila siku,inapakia mtu na mizigo midogo isiyozidi kilo 50.
Ushauri wangu tafuta rimu za pikipiki za kijapan,hata hiyo shockup kati tafuta ya 250 baja funga
 
Bila shaka umeshakaa nayo miezi kadhaa sasa. Naomba experience, ipoje? nafikiria kununua pia.
Binafsi, nimetumia hii Sinoray 250cc ADV kwa muda kidogo, uzoefu wangu mdogo ni huu.
1. Matumizi ya mafuta
Ipo vizuri kwenye matumizi ya mafuta, huwa naenda wastani wa km 100+ kwa lita 4.
2. Upatikanaji wa vipuri.
Napata vipuri kwa uhakika kabisa na gharama ni rafiki.
3. Uendeshaji
Ni pikipiki nzuri sana ukiwa kwenye barabara ya lami. Changamoto yake kubwa ni kwenye ugumu wa siti.( Lazima makalio yaume ikiwa unatumia kwa safari ndefu)
Pia, huwa inatengeneza joto sana kwenye "foot rest" upande wa kulia.
Unapokuwa kwenye barabara za vumbi, changarawe, mchanga mwingi, jaribu kuwa makini sana kwani "stability" yake ni ndogo sana.
 
Nimenunua sinoray ADV 250CC naona shokapu za mbele na ile ya nyuma ngumu sana, kwenye mabonde badala ya kunesa inakuwa inadunda tu.

kuna namna ya kurekebisha shokapu ziwe zinanesa? hasa rough road zenye mabonde unakuwa hupati ule mneso.

Kngine kwenye mchanga mwingi inayumba sana, kuna namna ya kufanya kuifanya iwe stable?

Ahsante nawasilisha.
Kuna jamaa yangu mmoja hiyo pikipiki imemtesa sana na maumivu ya mgongo kama mwezi hv kazunguka hospital nying kujua shida nn lkn kachemka. Juzi nakutana naye ananiambia baada tu ya kubadilisha shockup akajikuta amepona mgongo na amesahau kabisa maumivu. Hizo pikipiki zina shockup ngumu sn nafikiri zipo kisport zaid na sio luxury
 
kuna msukuma mmoja katoka mwanza kaja kununua hiyo chuma dar, mpango wange ni kuendesha mpaka mwanza na alikua anatoa mrejesho hatua kwa hatua pale insta mambo yamemuendea vibaya sana, nadhani wahusika wafanye namna ya kuboresha .

nakala kwa Xi Jinping
 
Kuhusu kuyumba sana kwenye mchanga:

Hapa kuna jambo muhimu: Sinoray yako ina front tyre 90/100-21, ambayo ni nzuri kwa off-road, lakini bado ni pikipiki nyepesi akriban kilo 145 na wheelbase yake ni 1,330 mm

Kwa hiyo kwenye mchanga laini, hasa ukienda polepole sana au ukiushika handlebar kwa nguvu, front wheel inaweza kutafuta njia yake na kuonekana kama inayumba

Usijaribu kurekebisha hilo kwa kufanya suspension iwe ngumu zaidi. Badala yake

Pressure ya tairi ni muhimu sana kwenye mchanga, lakini usiweke pressure fulani kwa kubahatisha bila kujua specification ya tyre yako

Angalia sticker/manual ya pikipiki au sidewall ya tyre. Mpelekee fundi:

Kwanzs apime rider sag mbele na nyuma. Rear preload iwekwe kulingana na uzito wangu.

Kisha itest kwenye rough road. Kama bado inaruka baada ya bonde, apunguze rebound damping kidogo. Mbele pia iangaliwe kwa fork oil na damping.

Halafu acheck tyre pressure na wheel alignment

Muhimu zaidi: badilisha kitu kimoja kwa wakati mmoja, kisha test. Ukibadilisha preload, oil, tyre pressure na rebound kwa wakati mmoja hutajua ni kipi kimeleta improvement
 
Binafsi, nimetumia hii Sinoray 250cc ADV kwa muda kidogo, uzoefu wangu mdogo ni huu.
1. Matumizi ya mafuta
Ipo vizuri kwenye matumizi ya mafuta, huwa naenda wastani wa km 100+ kwa lita 4.
2. Upatikanaji wa vipuri.
Napata vipuri kwa uhakika kabisa na gharama ni rafiki.
3. Uendeshaji
Ni pikipiki nzuri sana ukiwa kwenye barabara ya lami. Changamoto yake kubwa ni kwenye ugumu wa siti.( Lazima makalio yaume ikiwa unatumia kwa safari ndefu)
Pia, huwa inatengeneza joto sana kwenye "foot rest" upande wa kulia.
Unapokuwa kwenye barabara za vumbi, changarawe, mchanga mwingi, jaribu kuwa makini sana kwani "stability" yake ni ndogo sana.
Shukran kaka
 
Kuhusu kuyumba sana kwenye mchanga:

Hapa kuna jambo muhimu: Sinoray yako ina front tyre 90/100-21, ambayo ni nzuri kwa off-road, lakini bado ni pikipiki nyepesi akriban kilo 145 na wheelbase yake ni 1,330 mm

Kwa hiyo kwenye mchanga laini, hasa ukienda polepole sana au ukiushika handlebar kwa nguvu, front wheel inaweza kutafuta njia yake na kuonekana kama inayumba

Usijaribu kurekebisha hilo kwa kufanya suspension iwe ngumu zaidi. Badala yake

Pressure ya tairi ni muhimu sana kwenye mchanga, lakini usiweke pressure fulani kwa kubahatisha bila kujua specification ya tyre yako

Angalia sticker/manual ya pikipiki au sidewall ya tyre. Mpelekee fundi:

Kwanzs apime rider sag mbele na nyuma. Rear preload iwekwe kulingana na uzito wangu.

Kisha itest kwenye rough road. Kama bado inaruka baada ya bonde, apunguze rebound damping kidogo. Mbele pia iangaliwe kwa fork oil na damping.

Halafu acheck tyre pressure na wheel alignment

Muhimu zaidi: badilisha kitu kimoja kwa wakati mmoja, kisha test. Ukibadilisha preload, oil, tyre pressure na rebound kwa wakati mmoja hutajua ni kipi kimeleta improvement
Safari hii kapiga mwanza - dar
Naona chuma haijamsumbua

View: https://www.instagram.com/reel/Dd6-QHcRQrn/?stkn=OWl2OHVlcm5yN3Zj
 
Back
Top Bottom