Nimenunua kisimbuzi ya startimes vip ligi ya wingereza nitaona?

Nimepata pesa fulani hivi huku ikitosha kununua startimes vipi nitaangalia gem ligi zipi na zipi maana lengo nione man U Asenal, Liverpool, etc.. Nipo njiani naenda kufunga sasa
Utafurahia ndondo cup lakini siyo Soca.
 
Kila juma mosi utaona mechi Moja ya ligi ya uingereza epl inarushwa na k24 chanel namba 288, Kuna sanyuka tv channel namba 403. Utaangalia ligi ya ujerumani, ufaransa, utiruki, uarabuni, mechi zote za CAF, Ligue ya Kenya, Uganda, Ghana na Nigeria baadhi.

Ili kufaidi hayo lipia kifurushi Cha elf 21. Karibu startimes
 
Nashukuru mkuu
 
Nikupe ushauri, kabla hujanunua bidhaa yoyote hakikisha ina huduma unazozipenda. Kuna simu, kompyuta, tv na kadhalika. Visimbusi viko vingi na vinatofautiana huduma baadhi. Kuna chaneli hazipo kwenye visumbusi fulani. Makampuni mengine ya utangazaji yana visimbusi vyao na wameweka chaneli zao na zingine ila kuna washindani wao kibiashara nao wana chaneli zao na zingine. Hawa wote wana wateja wao wa kununua visimbuzi vyenye chaneli wanazozihitaji
 
Sasa si ungeuliza kabla ya kununua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…