Nimenunua mzigo toka china kupitia ebay track number inaonesha umefika ila posta haupo

Nimenunua mzigo toka china kupitia ebay track number inaonesha umefika ila posta haupo

ommy15

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
674
Reaction score
1,017
Habari wanabodi. Kabla sijafika mbaki napenda kuwashukuru wote mliotoa michango yenu kuhusu manunuzi kwa njia ya mtandao. Kweli mimi binafsi nimefaidika sana na michango na nyuzi zenu Mungu awabariki wote.
Lengo la uzi huu ni kwamba nilinunua hand bag china kupitia ebay ambayo kwa track number inaonesha umefika Tanzania siku zaid ya 20 zilizopita na nikienda posta wanasema haujafika hapo ndio nashindwa kuelewa kwamba utakuwa wapi na hapo nililipia na usafiri kwani free shipping ndio inachelewa sana.
Pia kwa wale ambao bado hatujaweza kununua vitu kwanjia ya mtandao kusema kweli ni nzuri na bei ni nzuri sema shida ndogo ndogo zipo hasa kuchelewa mzigo wako,kutotumwa kabisa ila hapa nashukuru Paypal wako fasta kwenye kurejesha fedha coz nimerudishiwa zaid ya mara mbili mwanzo nilinunua viatu na nguo na havikutumwa nikadai na hela ilirudi. Na nmenunua vitu vingi bei nzuri mfano saa za dola 5 huko nje huku kwetu bei yake ni zaid hata ya mara 3.
Asanteni
IMG_20171216_205005_565.JPG
 
I had the same prob.... Toka Sept mzigo unaonekana umefika lakini sijapata mpaka leo, nilishaclaim ebay nikawa refunded
 
Nijuavyo iko hivi Kama uko mkoani mzigo ukifika dsm unapokelewa then wanasort mzigo kwanza ili kutumwa katika office ya posta iliyopo karibu na wewe, kama una number ya item nenda Kwenye website ya posta Kuna sehem ya Kutruck utaingiza hiyo item number utajua mzigo uko wapi office gani na umepokelewa na nani nikimaanisha mhudumu aliyepokea mzigo siku hiyo ulipoingia
 
Umeokoa gharama kiasi gani mana kuna wengine ni wa tz wanaouza huko ebay
 
Wahudumu wa posta wamesha upiga... Wabongo ni wezi sana, hadi Magufuli akawakurupushe ndiyo akili iwakae sana
 
Asanteni wadau kwa michango yenu na samahani sikuwa hewani muda kidogo kuwajibu. Mzgo nmefanikiwa kuupata ila nilichojifunza wafanyakazi wa posta hawajui wanatakiwa kufanya nini. Kwani mzgo ulifika dar tar 11 mwez wa 11 na kufika mbeya ni ndani ya wki moja. Shida iko pale posta mbeya yaani wale wamama hawajui wanachofanya kwani kila nikienda njoo baadae njoo kesho. Hadi mwena zaid umepita
 
Basi thread closed! Hongera kwa kupata mzigo
 
Back
Top Bottom