Nimenunua 'novel' ya Kiswahili nikakutana na neno 'Tafadhari' hapa naenda kudai refund

Cicero

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2016
Posts
2,924
Reaction score
3,074
Kama mtu aliyekulia nje na mwenye nia ya kuboresha Kiswahili changu, si nikaamua ninunue novels za Kiswahili ili zinisaidie.
Yaani nimefungua tu ukurasa wa kwanza nikakutana na hilo neno hapo juu "TAFADHARI".
Hivi muandishi mzima uliyeenda shule unaweza kukosea lugha kiasi hicho. Uandishi wa namna hii ni janga kwa taifa letu na unatakiwa kupigwa vita naona watu wengi mno ni wahanga.
ELIMU ELIMU ELIMU.
Hapa niko njiani naenda kurudisha mtabu wao!
 
Nakuunga mkono kirudishe na udai chako, shenzy type huyo mwandishi atakuwa kabila moja na Yule wa magogoni ~"nitarara nao mbere" nonsense sipendi makosa ya kipuuzi namna hii kwenye maandiko!
 
yaan ukarudiwe hela yako mkuu haraka saana hicho sio kiswahili ni kiwahili
 
Nakuunga mkono kirudishe na udai chako, shenzy type huyo mwandishi atakuwa kabila moja na Yule wa magogoni ~"nitarara nao mbere" nonsense sipendi makosa ya kipuuzi namna hii kwenye maandiko!
Huo mfano wako haujasadifu. Kisukuma hakina kimadende /-r-/ na kinapohitajika wao huweka /-l-/ mahala pake. Wakurya wao ni kinyume chake....
 
'novel' ya kiswahilii hakuna mkuu mbona hata wweee unamakosa ya kisarufi
 
Nimecheka sana aisee. Ongezea na madai ya kukusababishia msongo wa mawazo na kukuumiza kisaikolojia😀😀😀
 
Kama mtu aliyekulia nje na mwenye nia ya kuboresha Kiswahili changu, si nikaamua ninunue novels za Kiswahili ili zinisaidie.
Yaani nimefungua tu ukurasa wa kwanza nikakutana na hilo neno hapo juu "TAFADHARI".
Hivi muandishi mzima uliyeenda shule unaweza kukosea lugha kiasi hicho. Uandishi wa namna hii ni janga kwa taifa letu na unatakiwa kupigwa vita naona watu wengi mno ni wahanga.
ELIMU ELIMU ELIMU.
Hapa niko njiani naenda kurudisha mtabu wao!

Wewe umeona kosa katika neno moja lakini wakati huo huo ukitoa malalamiko yako maneno mawili umeyakosea "muandishi " "mtabu"
Acha nasisi tumwambie mod. Aifute hii post yako.
 
Mkuu tupe jina la hicho kitabu na mwandishi wake na kinapatikana wapi
 
Back
Top Bottom