Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,801
- 4,212
Hakika hakuna kitu nachukia kama watu kutumia lugha kipuuzi kabisa. Bora kabisa kawadai na ikibidi tuwafungulie kesi kwa kutokuitunza tunu ya Taifa.Kama mtu aliyekulia nje na mwenye nia ya kuboresha Kiswahili changu, si nikaamua ninunue novels za Kiswahili ili zinisaidie.
Yaani nimefungua tu ukurasa wa kwanza nikakutana na hilo neno hapo juu "TAFADHARI".
Hivi muandishi mzima uliyeenda shule unaweza kukosea lugha kiasi hicho. Uandishi wa namna hii ni janga kwa taifa letu na unatakiwa kupigwa vita naona watu wengi mno ni wahanga.
ELIMU ELIMU ELIMU.
Hapa niko njiani naenda kurudisha mtabu wao!