Nimenunua 'novel' ya Kiswahili nikakutana na neno 'Tafadhari' hapa naenda kudai refund

Hakika hakuna kitu nachukia kama watu kutumia lugha kipuuzi kabisa. Bora kabisa kawadai na ikibidi tuwafungulie kesi kwa kutokuitunza tunu ya Taifa.
 
Mkuu hiyo ni novel tu.. Nenda kwenye vitabu vya ziada vya mashuleni huko ndo utakimbia.. Unaweza kukutana na kitabu kwenye maswali ya mazoezi kumeandikwa rais wa awamu ya kwanza wa tanzania anaitwa (a) mkapa (b) mwinyi (c) kikwete. Afu unakutakipo shuleni kinatumika kufundishia ndo utashangaa..
 
Mimi bado najifunza ila huyu ni MWANDISHI mzimaaa! Aibu sana.
Sawa kabisa.
Ni vyema na wewe uboreshe, ukikosoa basi weka jitihada na wewe kwa upande wako.

N.b.
Inawezekana makosa ya kiuandishi sio yake bali ni ya mchapishaji. Mpe nafasi. Soma kitabu, kielewe na kama kinaeleweka unaweza kutoa mrejesho kwa manufaa ya mwandishi na wapenzi wa kusoma vitabu pia. Naamini kuna mawasiliano ya mwandishi na/au mchapishaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…