Nimeokota sarafu yenye tundu katikati ya 1918

Nimeokota sarafu yenye tundu katikati ya 1918

EL ELYON

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
1,565
Reaction score
1,918
Wakuu mmebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu.
Nimeokota sarafu yenye tundu KATIKATI imeandikwa EAST AFRICA & UGANDA PROTECTORATES ( ONE CENT )
SHIDA YANGU JE HII KITU INA THAMANI YOYOTE KWASASA MAANA NILIWAHI SIKIA WATU WANASAKA PESA ZA NAMNA HII.

0629 945 110.
IMG_20220612_160446774.jpg
IMG_20220612_160432474.jpg
 
Hizo enzi zetu ziliitwa Kibaru. Baada ya kukosa thamani zilikuwa zinavaliwa na mabibi kama urembo wa kizamani, mara nyingine nilikuwa naona wanawavalisha watoto wachanga kiunoni sikujua maana yake
 
ndugu, mpaka hapo tuseme ushatoboa, hiyo ni moja wapo ya hazina za mjerumani

mpaka nakuoneona wivu mzee, hapo sio chini ya million 77 unayo
🤔 Ngoja nione mwisho wake niifadhi tu kwanza maana humu kila mtu na mtazamo wake.
 
Hiyo labda upelekee waganga uswahilinibhuko tandale, buguruni, tandika, buza n.k
Naona huvalisha watoto shingoni na viunoni sijui ndio dawa ya nini?
 
google tu thamani yake, unaweza kuiuza kwa bei nzuri kwa wanaotunza vitu vya kale huko ulaya. ila bongo jau tu utaishia kupewa buku 2
 
Hivi zile 500 za zamani na zenyewe zina ishu yoyote??
 
Mpaka umeokota maana yake imetupwa na aliyeitupa ameona haina Cha maana na wewe itupe tu.
Mbona unamvunja moyo mdau /kuna haja ya kuwa na paypal kwa Tanzania yetu, vitu kama hivi unatangaza na unauza popote duniani na Pesa yako inaingia kwenye simu yako
 
ndugu, mpaka hapo tuseme ushatoboa, hiyo ni moja wapo ya hazina za mjerumani

mpaka nakuoneona wivu mzee, hapo sio chini ya million 77 unayo
Ooh, kumbe King George alikuwa mjerumani! Kwa mtindo huu ndiyo maana CCM inaendelea kutawala bila kutegemea kura.
 
Back
Top Bottom