Nimeombwa Ushauri na rafiki yangu kuhusu wasichana wake wawili

B! aolewe mapema sana anasifa zote za kuwa wife material na kasoro zake zinabebeka tu.
 
Kama ni lazima aoe hao B ndio Ana faa

Kwanza ndio ambae yupo kwenye mahusiano

Pili Ana sifa nyingi njema kuliko kasoro zake

Ana onekana ni wife material kuzidi A

ila A anaonekana ni mchunaji yupo kwa mwamba kwa maslah kifup Ana act love Ata kule kujituma kitandani ni trick tuu ya kumkoreza jamaa

Mimi hapo ninge chukua B Ata kama Ana sura ya Baba
 
Vijana wanasemaa " wapelekee moto tuuu mpka akili ziwakae sawa
 
Nipe na wewe sifa zako!
 
Asante kwa ushauri nitafikisha
 
Huyo jamaa yako anampenda yupi kati ya A na B, maana inawezekana B ana unafuu kimaelezo na A kuwa kilaza lakini penzi likawa limeangukia kwa kilaza.
 
Jamani asikuambie MTU, ndoa ni ngumu sana, zinawashinda hadi wasomi wenye PHD. Ndo maana haishangazi kukuta mume ana PHD na mke ana MASTERS lkn cha ajabu ndoa inakuja kuvunjwa na mwendesha bodaboda au Mangi wa pale dukani( Just mifano tu ). Hii yote ni kwa sababu kuungana kwa mwanamke na mwanamume kuwa mwili mmoja kunabebwa zaidi na UPENDO. Ndoa nyingi zimejaa MARYONGORYONGO (Mikwaruzo,migogoro) kwa sababu ya upendo kutokidhi matarajio ya aidha pande zote au upande mmoja. Kwa maana hiyo, Best yako anapaswa kuuliza moyo wake ni yupi kati A na B anapaswa kumuoa, uwe makini utakapo kuwa unampa ushauri ulioutoa hapa jukwaani maana ndoa ni ndoano, kuna watu walikuwa na ndoa zao lkn mwisho wasiku zilijaa maji na kugeuka kuwa ndoo, utalaumika sana kwa ushauri wako uliouokota toka hapa jukwaani na pengine utabeba dhambi zisizokuhusu (ingawa sikuombei iwe hivyo), maana hata we we umekiri kabisa kuwa ulishindwa kumshauri ndo maana umekuja kuomba usaidiwe kutoa ushauri ndo umpelekee. Nimeyaeleza haya kutokana na uzoefu wangu wa kuona ndoa nyingi zikidumu na kuparaganyika pia. Mimi ni MUME na BABA wa familia. Mnisamehe kama nimemkwaza MTU maana haya ni mawazo yangu tu!
 
Asante dada kwa ushauri mzuri wa kujenga kwangu na kwa muhusika. Barikiwa sana my dada, mwaaaaaaaa
 
Huyo jamaa yako anampenda yupi kati ya A na B, maana inawezekana B ana unafuu kimaelezo na A kuwa kilaza lakini penzi likawa limeangukia kwa kilaza.
Ndicho nilichokiona na mimi, ni kama kwa kilaza penzi ni moto ila B kawaida. Mwisho wa siku atachagua mwenyewe kwakweli maana mambo ya mapenzi yasije sutwa siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…