Nimeona aibu kwa niaba ya master aliyepigwa na mtoto

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wadau kuna ligi ya kick boxing inandelea Azam Sports, kwa sasa kila Alhamisi kuna mapambano. Alhamisi iliyopita kuna masta mmoja ambaye wanasema ni mkali wa Kung Fu, Shaolin na Gujuluu aliingia kupambana na kijana mdogo, master akagongwa knock out

Ushauri kwa ma-masta wengine aisee watoto ni wakali, unaweza kuwa master kwa maana kuwa una skills nyingi, lakini vijana wakakushinda nguvu, ni vyema wabaki kuwacoach vijana na sio kuingia ulingoni mzee akaaibika.

Honestly sijapenda hata waliomkubalia masta yule aingie ulingoni kupambana na mwanafunzi na mwanafunzi alionekana kuleta heshima lakini baadae akapiga moja master kaenda chini chaliii akasarenda.

Kwa ligi inayoendelea, msiwaweke mamasta tunawashushia heshima, ushindi ni probability.
 
Nidahamu katika martial arts imepungua sana. Sheria na taratibu za martial arts haziruhusu michezo hii kutumika kwaajili ya biashara au kujipatia kipato kwa namna yoyote ile, au kwaajili ya sifa au kufanyia uhalifu.

Mambo yamebadilika sana, kipindi tunasomewa historia ya kung fu na lengo kuu la kujifunza mengi yalikuwa nia njema.

Leo hii mtu akijua unacheza michezo hiyo anaanza kutazamia tofauti kabisa na wengine mpaka kufuatilia na vyombo vya ulinzi.
 
Kuna tofauti ya master wa China na wa bongo. Kule China kadri master anapozeeka ndiyo anakuwa fit, ila Bongo master akisogea umri kidogo tu anakuwa mlenda mlenda.
 
Wacheza kick boxing na boxing wanawasumbuaga sana mamaster,nenda youtube kule uone ma master wavyotolewa ushuzi kwenye real chalange sparing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…