Nimeona bendera za Taifa nusu mlingoti maeneo ya round about za Posta, kulikoni?

Nimeona bendera za Taifa nusu mlingoti maeneo ya round about za Posta, kulikoni?

RWANTANG

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2021
Posts
1,143
Reaction score
1,425
Habari wana JF kama kichwa cha bandiko kinavyosomeka kulikoni bendera nusu mlingoti?
 
Habari wana JF kama kichwa cha bandiko kinavyosomeka kulikoni bendera nusu mlingoti?
... nchi iko salama Mkuu; ni ujirani mwema na Kenya tunaomboleza pamoja nao msiba wa Rais wao mstaafu Mwai Kibaki.
 
Unatuzuga tu,ulifikiri ni kitu kizito cha hapa nchini
... Mkuu ingekuwa kitu kizito cha hapa hata watoto wadogo wangejua maana tv na radio stations zote habari ingekuwa ndio hiyo. Mungu aepushe mbali.
 
Kenya ni ndugu zetu damu nao huwa wanalia nasi hata asipofariki Magufuli walishusha bendera siku mbili
 
... Mkuu ingekuwa kitu kizito cha hapa hata watoto wadogo wangejua maana tv na radio stations zote habari ingekuwa ndio hiyo. Mungu aepushe mbali.
Haaaaaaaa,hata Chanel ambazo huwa BAD SIGNAL zingeonesha
 
Ila namna hii serikali awamu sijui ya 6 inavyoendeshwa inatia mashaka makubwa!

Msiba wa Mwai Kibaki wa Kenya umetokea takribani wiki moja sasa imepita, eti leo ndio serikali yetu inakurupuka kana kwamba ilikuwa imelala usingizini kukumbuka habari ya bendera kupepea nusu mlingoti kama heshima kwa majirani zetu hao.

Ina maana Majaliwa au Dr Mpango kwann hawakumkumbusha Mama akiwa nje ya nchi kwenye Royal Tour kwamba majirani wamepata msiba na hivyo Mama angeagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa wakati sahihi (naamini kuanzia siku ya pili tu toka tutangaziwe msiba huo) kuliko hiki wanachokifanya sasa hv.

Kwakweli viongozi wetu wanatia mashaka sana hasa kwa watu makini kama kweli wapo organised!!!.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom