Ila namna hii serikali awamu sijui ya 6 inavyoendeshwa inatia mashaka makubwa!
Msiba wa Mwai Kibaki wa Kenya umetokea takribani wiki moja sasa imepita, eti leo ndio serikali yetu inakurupuka kana kwamba ilikuwa imelala usingizini kukumbuka habari ya bendera kupepea nusu mlingoti kama heshima kwa majirani zetu hao.
Ina maana Majaliwa au Dr Mpango kwann hawakumkumbusha Mama akiwa nje ya nchi kwenye Royal Tour kwamba majirani wamepata msiba na hivyo Mama angeagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa wakati sahihi (naamini kuanzia siku ya pili tu toka tutangaziwe msiba huo) kuliko hiki wanachokifanya sasa hv.
Kwakweli viongozi wetu wanatia mashaka sana hasa kwa watu makini kama kweli wapo organised!!!.
Sent from my SM-J530F using
JamiiForums mobile app