Nimeona daraja la waya (cable stayed bridge) la SGR Kamata likivunjwa, shida nini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Pale Kamata kuna daraja la kupitisha treni ya SGR lilikuwa linajengwa (Cable stayed bridge) ambapo ile minara miwili inayoshika waya (cables) ilishakamilika.

Ila cha kushangaza, jana nilipopita pale nimekuta mnara mmoja ukiendelea kuvunjwa, kwa mnaofahamu, nini kinaendelea?

==================================
Update: 12/10/2020

 
Toka lini umekuwa mhandisi? Kwani shida iko wapi? Mlisema mkiingia ikulu mnabomoa reli madaraja na flyover! Sasa tumeanza kubomoa hilo la kamata mbona tena unachukia? Tar 28 kura zote kwa magu
 
Mimi kwa kuliangalia tu nilihisi lina makosa, niliona kabisa pale treni haziwezi kupishana.
Kazi za ujenzi ni kazi pekee ambazo hata wasio wataalamu wanaweza kukosoa
Kwani ile si reli ya njia moja au? Na treni hupishana kwenye vituo maalum vya kupishanishia treni au?
 
Toka lini umekuwa mhandisi? Kwani shida iko wapi? Mlisema mkiingia ikulu mnabomoa reli madaraja na flyover! Sasa tumeanza kubomoa hilo la kamata mbona tena unachukia? Tar 28 kura zote kwa magu
Walisema akina na nani hadi unijumuishe? Unataka kujua kama mimi ni mhandisi?
 
Kwenye mradi mkubwa kama huu kubomoa na kurekebisha baadhi ya maeneo ni jambo la kawaida sana. Hongera kwa kufuatilia maendeleo ya mradi huu unaojengwa kwa kutumia kodi za Watanzania wote.
 
Huu mradi tuliambiwa unakamilika mwaka jana na Treni ya kwanza ingefika Moro Nov. 2019. Hadi sasa kila mtu kimya. Mradi umesha fail kabla haujaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…