Nimeona hapa ndo kuna shida kwa vijana wengi Tanzania

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Habarini wadau. Nlikuwa na mizunguko kidogo ya kikazi.Canada,Egypt,Sweden,South Africa na Kenya.

Nipo bongo. Nmesikitika leo kukuta jamaa wanagombana sababu ya tsh 100,000 tu.hii hii ya madafu.jamaa mmoja aliazimwa pesa hiyo sasa mwaka wa pili hajarudisha na namba akachange.leo kakutana na mdai hapa M.City. Ndo ikawa Issue.

Tunakwama sana.100,000 si pesa.si pesa ya kuvunja urafiki.lakini watanzania wengi hawajui maana ya kukopa na kuomba kupewa.

Mwaka jana nlikuwa sehemu na jamaa nmemtoa out.Hotel moja ufukweni. Naye akamwita Girfriend wake mpya amwoneshe yeye matawi.nikalipia bill yangu nikawa naaga. Jamaa akashtuka maana ndo wakati huo huyo dada amekaa tu. Mimi nliona niwaachie nafasi.
Akanambia nimsubiri anisindikize.akanifuata kwenye Jeep na kuomba nimkopeshe tsh 200,000. Atanirudishia.nikavuta draw nikahesabu nikampa.

Mwisho wa mwezi nikamkumbusha jamaa.akaanza kunambia sijui alikuwa na makato mengi na hadithi nyingi sana.nilimwambia hayo sasa yanahusiana nini na pesa yangu.akaanza kucheka cheka na kudai mimi nina pesa nisimdai hiyo 200,000.nlimwambia alikopa which means anapaswa arudishe.

Akakwepa kwepa miezi ikaisha.hakurudisha.juzi nmerudi amekwama.anataka nimkopeshe tsh 1,800,000. Nikamwambia arudishe kwanza ile 200,000. Akapita siku moja ya pili akaniletea ile pesa.

Nilipopokea nikaiwapa walinzi wagawane. Akanambia sasa inakuaje lile ombi lake. Nilimjibu tu sina.

Imekuwa issue ofisini.analalamika sana kuwa nmemfanyia ubaya.ubaya wangu ni upi hapo? Anadai namiliki magari makali lakini nmemnyima mkopo mdogo tu kama huo aongezee kweye kodi.nikashangaa sana.magari ni yangu,pesa ni yangu.sijamdhulumu why anivishe ubaya?

Vijana wa tanzania tunakwama ,tunapoteza imani,tunapoteza uaminifu kwa mambo madogo.tunapenda makuu. Siku ile nimemtoa out yeye.naye anamwita girlfriend wake...huku hana pesa.why?
 
Thread zako zimeanza kupoa sana mkubwa au labda nyingine hatuzioni kwa sababu ya kichaa cha mamods
 
[emoji23][emoji23][emoji23] eti 100,000 pesa ya madafu! Wengine hiyo pesa ni mshahara wake wa kazi eti! mm hata niwe na billions of money kama ulikopa hela yangu ukanilipa hata ibaki Tsh 50 nakudai maana nihaki yangu bado unayo lazima unilipe.

Hao wakina Mo & SSB mabilionea lakini wanatengeneza bidhaa hadi za shilingi 50 hawataki hata zibaki mifukoni mwetu alafu mm ni nani nisidai tsh 50!
 
Dogo ulipotea sana
 
Huu Uzi wako utapelekwa jukwaa la malalamiko maana ndio ulioanza nayonayo, usiwalaumu mods ni makosa yako.
 
Kuna mtu ananipaga pesa nyingi tu millions kadhaa.
Juzi nilikwama laki 4 nadaiwa.
Aiseeee ikabidi nimuingie anikopeshe.
Akanikopesha.
Lakini najua hiyo hela kwake hawezi nidai na ni hela upande wake ni ya kuspend ijumaa usiku, napengine haitoshi.
Lakini ni lazima nimlipe maana kanikopesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hivyo maisha kusaidiana sasa kama hutarudisha atapata wapi huo moyo wa kusaidia wengine? maana atakuwa kaingia kinyongo tena hatowaamini na wengine pia.
 
Mie nishakopwa na majirani wote, wanalipa wanavyojisikia wao, wengine mwaka wa tatu hawajalipa Jan. iliyopita wanakuja niwakopeshe, kwanza nikakubali ila nikamwambia anisubiri kama siku tatu, zikapita siku tatu kwenye simu ikawa kama deni! Asubuhi naamka na sms yake, lunch simu, jioni hadi usiku kwa siku mbili mfululizo, nikampigia siku ya sita kumwambia mipango yangu imefail so sitakuwa na uwezo wa kumsaidia. Kanuna balaa, jana tumekutana sehem ya manunizi ya mahitaji kajifanya hajaniona nami nikala jiwe. Kukopeshana bongo ni kuua urafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…