Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hatari sana.Kuna mtu ananipaga pesa nyingi tu millions kadhaa.
Juzi nilikwama laki 4 nadaiwa.
Aiseeee ikabidi nimuingie anikopeshe.
Akanikopesha.
Lakini najua hiyo hela kwake hawezi nidai na ni hela upande wake ni ya kuspend ijumaa usiku, napengine haitoshi.
Lakini ni lazima nimlipe maana kanikopesha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ndugu zangu fulani, kadhaa, na waliokuwa marafiki, kadhaa, nimewapoteza kwa sababu ya mikopo.
Yani unamkopesha mtu, halafu huo mkopo mdogo tu ndio unakuwa sababu anakomesha urafiki nawe, mwingine ndugu kabisa lakini kakopa, hataki kulipa, na anakukwepa kwa sababu ya mkopo. Kuna watu sijaongea nao sasa zaidi ya mwaka wa pili, kwa sababu ya mkopo mdogo tu.
Sasa hapo mtu anapata mtihani mgumu sana, mara nyingine naona bora niseme sina hela, ili mkopo usije kunikosesha ndugu, jamaa na marafiki.
Lakini mara nyingine, unaangalia mtu ana shida, unaona imani, unaamua ngoja nimpe tu, akinifanyia ubaya kutolipa ni ubaya wake yeye.