Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nyc storiSongíto;3801902 said:unankumbusha swaiba wangu mmoja nae kamaliza ud 2006... alikuwa na mdada mmoja ambaye kwao unaweza kusema ndipo zinapotengezezwa noti nadhani mnanielewa namaanisha nn... jamaa yeye alikuwa kama wenzangu na mimi, nyumbani kawaida sanaaaa..... walidumu na yule dada miaka tisa kwenye mahusiano.... kila mtu aliwachukulia kama mfano wa kuigwa kwenye mahusiano, maana walipendana na walishibana haswa... walipitia vikwazo vingi sana ikiwa pamoja na kukataliwa na wazazi wa dada lakini bado walimudu... ajabu wakati wametafuna ng'ombe wote umebaki mkia dada akamwaga yule kaka wakiwa mwaka wa mwiso chuoni udsm, na walipanga soon wakimaliza wafunge ndoa... kaka aliugua akalia akawa hana hamu... ikawa ibada kwa sana, na kuokoka akaokoka...
katika kuokoka kwake akaoteswa ndoto kama yako kuwa kuna mdada anamtoke na kumwambia kuwa yeye ni mwenza wa maisha... ajabu na mama huko kijana pia akaota ndoto kama hiyo kwa msichana huyohuyo sema aliota wamefunga ndoa tayari na mwanae..... jamaa akajiambia kama ni yeye ntampata tu.... walikutana supermarket siku moja town and it was the same dat jamaa alimtamkia dada kuwa anampenda, na dada alikubali hapo hapo bila swali na sasa wamefunga ndoa wanaishi kigamboni dar es salaaa....
inaweza kuwa mungu anazungumza nawe pia kwa njia hiyo......
Jambo la kuomba ili upate mwenzi wako huwa wakati mwingine ni gumu na si rahisi sana kuamini miongoni mwa vijana wengi.Je ushawahi kuota ndoto yenye sauti elekezi? Hii ni aina ya ndoto ambayo mtiririko wote wa matukio katika ndoto huongozwa na sauti fulani,this is what happened to me! Wakati nasoma kidato cha nne siku moja nilioteshwa hii ndoto; nilioneshwa wadada wa3 wakiwa wamesimama,kiurefu dada wa katikati alikuwa mrefu kushida wale wawili wa pembeni yake,ile sauti elekezi ilinielekeza kwamba "wawili kati ya watatu hawa wataondoka" na kweli wale wadada wawili pembeni ya dada yule mrefu wakaondoka na hatimaye akabaki yule mrefu kuzidi wale wawili aliyesimama kati yao,ile sauti ikanijia tena na kuniambia"huyo aliyebaki hapo ndiye atakayekuwa mke wako wa maisha" baada ya pale nikastuka kutoka usingizini.Tangu pale huwa namwomba Mungu anisaidie nimpate yule binti(mrefu,mweupe afu mrembo).nilipojiunga na chuo siku moja nilimwona yule binti,sijawahi kumuongelesha na cha ajabu huwa hana mpango na mimi hata interest kisalamu.kiniumizacho zaidi jamaa yangu huwa anamzungumzia yule binti na kusema kuwa si punde atamtokea,hilo linanipa headeche kwamba sijui nimuhawi au nizidi kusubiri nikijiaminisha kwamba jamaa atakataliwa nami nitamkaribia yule binti kwan itakuwa ni ishara mojawapo kuwa ni wangu!! (Nakaribisha maoni wadau!!)