Nimeota ndoto ya ajabu!

Kuna watu huwa wanaota ndoto zinakuwa kweli. Na ww ni mmojawapo?
Kuna ndoto kadhaa, nzuri na "mbaya" nilishawahi kuota na zikatimia. Lakini pia kuna nyingi nilishaziota nikaishia kuzipuuzia, kwamba zilikuwa ni ndoto tu na hazikuwa na madhara yoyote. Lakini ya leo imekaa kwa namna ambayo "ninashindwa" kuipuuzia.
 
Nivitu gani ulikuwa ukitafakari wakati ukilikagua shamba? Labda kufanya kitu fulani hapo n.k

Ni vitu gani ulikuwa ukitafakari kuhusu hilo shamba wakati ukirejea kutoka huko shambani?

Je safari Yako ilikuwa ndefu kufika huko shambani? Kulikuwa na vikwazo vyoyote njiani?

Ulitua shambani kwa matakwa Yako au Kuna nguvu ilikulazimisha kutua hapo??

Kwenye shamba hilo au maeneo ya jirani kulikuwa na shughuli yoyote ya kibiashara ilikuwa ikiendelea? Labda kilimo n.k

Umewahi kutafakari jambo lolote na likatokea?
 
Soma ASTRAL PROJECTION
 
ulivuta skanka ilochanganywa na ugoro!
 
wanga na wachawi wanataka kukutumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuwa msukule..

Omba na kukemea kwa bidii sana hiyo roho ya kichawi na kishirikina inayokuzengea.

watesi wako ni watu wanaokufahamu kabisa, wanataka kukupora nyota na ndoto ya mafanikio yako inayong'aa sana, wanataka kusambaratisha na kutokomeza uwezo wako, wa familia na ukoo wako katika nyanja zote.

That's alert for you to be careful, kuna jaribu kubwa linakujia na linaweza kua kama lile la Yesu alipopelekwa juu ya kilele cha mlima na Ibilisi, na kisha akaambiwa ajirushe, ikiwa kweli wewe ni mwana wa Mungu ๐Ÿ’
 
Kula vyakula laini usiku

Oga kabla ya kulala

Sali kabla ya kulala

Lala sehemu nzuri Safi na yenye hewa ya kutosha

Usishibe Sana usiku

Usiangalie movie usiku kabla ya kulala

Usilale na simu kitandani weka charge sebureni

Ukizingatia hayo hautaota ndoto na kuzikumbuka
 
Kuna ndoto nilishawahi kuiota na ikawa vivyo hivyo!
 
Ukifatilia kila ndoto hutakaa kwa amani
Usiku wa kuamkia leo nimeota zaidi ya ndoto moja, lakini ni hii moja tu ndiyo nimeiona ya kipekee. Na siku zingine pia huwa ninaota, lakini mara nyingi nilizipuuzia kwa kuwa zilikuwa "ndoto" tu!
 
Sure mkuu,kuna vitu vingine tunavipa attention ambavyo havina impact yoyote.
Lakini pia wakati mwingine kuna "vitu" vidogo watu wanaweza kuvipuuizia kumbe vingeweza kuwa na msaada mkubwa sana kwao kama wangejua yawapasayo!
 
1. Shamba lilinivutia nikawa natamani lingekuwa kubwa zaidi, kama ekari hamsini ili nifanye kilimo cha umwagiliaji. Hilo nililoliona lilikuwa na ukubwa kama ekari tano hivi.

2. Nilikuwa nikiwaza kwamba kama Mungu atapenda, nitalinunua hilo shamba. Pia nilikuwa najiuliza kwa nini sikuchunguza kando kando ya mto, labda ningeyagundua madini yaliyopo kwenye huo mto

3. Safari ilikuwa ndefu kwa kiasi fulani. Hakukuweko na kikwazo chochote. Kuna mahali nilikuta mti una matawi yaliyokaribiana na kuacha katikati yake upenyo mdogo ambao siyo rahisi mtu kuweza kupenya, lakini mimi nilipeya bila kuugusa na nikajua ni kwa sababu sikuwa kwenye mwili ndiyo maana sikushindwa kupita kwenye huo upenyo mdogo.

4. Sikujua kilichokuwa kinanifanya nielee hewani. Sikujua chini, hilo shamba nililiangalia nikiwa hewani. Inawezekana ningeweza kuendelea mbele zaidi lakini niliamua kurudi kwa kuhofia kuwa niliendelea kwenda mbele zaidi naweza nikashindwa kurudi nilikotoka, kwenye mwili wangu.

5. Hapana. Hilo shamba halikuwa na mazao yoyote zaidi ya miti, ila miti haikuwa imesongamana sana ingawa baadhi ya miti ilikuwa ni mikubwa sana. Sikuona mazao kwenye mashamba jirani ingawa kulikuwa na nyumba zilizotwanyika sana, zilikuwa mbalimbali sana, nyumba za tope zilizoezekwa kwa bati

6. Ndiyo, nilishawahi kutafakati jambo na likatokea, na nilishawahi kuota jambo na hiyo ndoto ikatimia.
 
Huenda safari yako ya maisha hapa duniani ingali fupi sana kuanzia sasa.
Please jikite kuwa humble
 
Tafakari hilo swali lako ulilomuuliza Mungu. Labda ni wakati sahihi wewe kuweka uwekezaji kwenye hiyo sekta ya madini. Angalia vigezo vyako kama vimetimia, fanya utafiti inawezekana unaonyeshwa njia.

Inaonekana una interest kubwa kwenye hiyo sekta sababu hata jina lako linaonyesha hivyo.
 
Ni kweli mkuu! Nina interest kubwa sana kwenye hiyo sekta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ