Nimeota ndoto ya ajabu!

Nimeota ndoto ya ajabu!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Ni ya ajabu kwangu! Sijawahi kuiota ndoto ya aina hii!!!

Nimeota nimetoka nje ya mwili wangu na kupaaa hadi eneo ambalo sikuwahi kufika, na hata sasa sipafahamu kama eneo hilo lipo au ni eneo la kufikirika tu. Lakini kama papo, nikipaona nitapakumbuka. Nilikariri baadhi ya maeneo, mfano, mti mkubwa, mto, na shamba lililopo kando ya mto.

Mwendo ulikuwa wa pole pole, na nilikuwa nikijaribu kukariri maeneo ili kama nikitaka kwenda nikiwa kwenye mwili niweze kupakumbuka. Nilikuwa najua kuwa sikuwa kwenye mwili.

Nilipoanza safari ya kwenda huko nilikokuwa nikienda, sikuwa najua nitakakoishia, wala sikujua lengo. Nilihisi kuwa labda ninaenda kuoneshwa eneo lenye madini kwa sababu kabla ya kulala, nilikuwa nikisoma makala mbalimbali za madini na vito vya thamani. Nilikuwa pia na shauku ya kuona mwisho wa hiyo safari. Nilikuwa nikiifurahia.

Maeneo niliyoenda ni ya vijijini. Nyumba zilikuwa chache, na ni za kivijijini (zimejengwa kwa tope zikaezekwa kwa bati), na zilikuwa mbalimbali sana.

Nilipofika penye shamba lililokuwa linaenda mpaka mtoni, nililitazama kwa muda kama vile nilikuwa nalikagua, kisha nikasema, "God, do you want me to buy this piece of land? Thank You". Kwa Kiswahili, (Mungu, unataka nilinunue hili shamba? Asante).

Nikiwa hapo mtoni, nilianza kuhofia kuwa nisije nikashindwa kurejea kwenye mwili wangu. Papo hapo niligeuza na kuanza kurudi hadi hatimaye nikajua kuwa sasa nimesharejea kwenye mwili wangu, na nikajitahidi kuamka.

Kwenye kuamka ilikuwa kama vile mtu aliyekamatwa na "jinamizi", lakini niliishinda hiyo hali na hatimaye nikaamka.

Nimejaribu kuitafakari hiyo ndoto lakini mpaka sasa sijapata mwanga!

Kuna anayeweza kusema "kitu"?

Asante!
 
Ungefika mwisho wa safari usingerudi tena kuna kipindi hizi ishu zilijadiliwa sana ila nikafuata ushauri wa Pascal Mayalla kuwa ukikosea ndio basi tena🐼

Tafsiri: Umeonyeshwa hazina yako ilipo.

Disclaimer:
Ila sasa kuifikia kimwili inaweza kuchukua hata miaka 60 au usifike kabisa maana siyo rahisi kwa mwanadamu kukaa kwenye viwango sahihi vya kiroho constantly bila kutetereka ndiyo maana wengi huforce kwa kutumia nguvu za ziada zinazoshirikisha kafara kinwa za damu kulipia gharama za huo 'uvumilivu na juhudi' zotakiwazo kufika huko.
 
Ni ya ajabu kwangu! Sijawahi kuiota ndoto ya aina hii!!!

Nimeota nimetoka nje ya mwili wangu na kupaaa hadi eneo ambalo sikuwahi kufika, na hata sasa sipafahamu kama eneo hilo lipo au ni eneo la kufikirika tu. Lakini kama papo, nikipaona nitapakumbuka. Nilikariri baadhi ya maeneo, mfano, mti mkubwa, mto, na shamba kubwa lililopo kando ya mto.

Mwendo ulikuwa wa pole pole, na nilikuwa nikijaribu kukariri maeneo ili kama nikitaka kwenda nikiwa kwenye mwili niweze kupakumbuka. Nilikuwa najua kuwa sikuwa kwenye mwili.

Nilipoanza safari ya kwenda huko nililokuwa nikienda, sikuwa najua nitakakoishia, wala sikujua lengo. Nilihisi kuwa labda ninaenda kuoneshwa eneo lenye madini kwa sababu kabla ya kulala, nilikuwa nikisoma makala mbalimbali za madini na vito vya thamani. Nilikuwa pia na shauku ya kuona mwisho wa hiyo safari. Nilikuwa nikiifurahia.

Maeneo niliyoenda ni ya vijijini. Nyumba zilikuwa chache, na ni za kivijijini (zimejengwa kwa tope zikaezekwa kwa bati), na zilikuwa mbalimbali sana.

Nilipofika penye shamba lililokuwa linaenda mpaka mtoni, nililitazama kwa muda kama vile nilikuwa nalikagua, kisha nikasema, "God, do you want me to buy this land? Thank You". Kwa Kiswahili, (Mungu, unataka nilinunue hili shamba? Asante).

Nikiwa hapo mtoni, nilianza kuhofia kuwa nisije nikashindwa kurejea kwenye mwili wangu. Papo hapo niligeuza na kuanza kurudi hadi hatimaye nikajua kuwa sasa nimesharejea kwenye mwili wangu, na nikajitahidi kuamka.

Kwenye kuamka ilikuwa kama vile mtu aliyekamatwa na "jinamizi", lakini niliishinda hiyo hali na hatimaye nikaamka.

Nimejaribu kuitafakari hiyo ndoto lakini mpaka sasa sijapata mwanga!

Kuna anayeweza kusema "kitu"?

Asante!
Inawe,a isiwe ndoto ila ni jambo lilitokea kweli. Kama sijakosea inaitwa astra projection
 
Ungefika mwisho wa safari usingerudi tena kuna kipindi hizi ishu zilijadiliwa sana ila nikafuata ushauri wa Pascal Mayalla kuwa ukikosea ndio basi tena🐼

Aisee!
 
Back
Top Bottom