Nimeota nimeokota 10,000 leo mwajiri kanitimua kazini

Nimeota nimeokota 10,000 leo mwajiri kanitimua kazini

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,730
Reaction score
9,088
UJUMBE KUTOKA KWA BINAMU YANGU.

Siku mbili tatu hizi, nilibahatika kupata kazi, kazi ya kusimamia apartments, kuangalia usafi, garden, luku, maji na vitu kama hivyo.

Usiku uliopita nimeota ndoto nimeokota 10,000. Leo boss kanipigia asubuhi kwamba jana alikuwepo apartments, na bahati mbaya gari ikamzingua, akakodi Ubber.

Wajibu wangu ulikuwa kumpeleka fundi wa gari, ahakikishe gari inawaka, pia kulikuwa na tatizo la umeme, Aletwe fundi umeme atengeneze.

Pia maji yalikuwa yamekatwa, ilitakiwa yarudishwe. Router pia ilitakiwa kuwa secured 🔐 maana siku chache nyuma mteja aliondoka na router.

Kazi nyingine ilikuwa ku replace nyavu madirishani. Kazi zote zimefanyika vyema na ilipofika saa 12 jioni boss akapiga simu anataka gari yake..

Apartments ni Bahari Beach yeye anakaa Mikocheni,. Nipokuwa nikimrudishia gari yake, (nilipita njia ya Tegeta Nyuki) bahati mbaya kwenye njia ya Wazo Hill nikakuta ajali mbaya ya gari la kubeba saruji.


Nimcheleweshea boss gari sababu ya foleni ya ajali, boss kakasirika sana kasema nimemtia hasara kubwa. Rasmi nimefutwa kazi.

Mungu wangu mwema, anajua haja ya moyo wangu , naamini hatiniacha mavumbini.
 
UJUMBE KUTOKA KWA BINAMU YANGU.

Siku mbili tatu hizi, nilibahatika kupata kazi, kazi ya kusimamia apartments, kuangalia usafi, garden, luku, maji na vitu kama

Mungu wangu mwema, anajua haja ya moyo wangu , naamini hatiniacha
Una uhakika hamna mlipokutana
 
Washangaze bwana washangaze weka tabasamu osoni mwangu ili wajue wewe unaweza.Zaidi ya yaliyoandikwa kwenye kitabu wewe Mungu.. Amiiiin
 
Back
Top Bottom