Nimeota zaidi ya mara tatu napigana na baba. Nini tafsiri ya ndoto hii?

Nimeota zaidi ya mara tatu napigana na baba. Nini tafsiri ya ndoto hii?

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Inakuwaje zaidi ya mara tatu naota napigana na mshua😂, yaani tunapigana sana na mawe wakati mwingine namhurumia lakini na yaye ananitupia mawe inabidi na mimi nimrushie.

Yaani tunapigana sana 😭, ni ndoto ya kujirudia pamoja na kuwa tuna mahusiano mazuri.

Tafsiri tafadhali.

1721180147554.png

Baba yako yaweza kuwa kuna jambo la kiroho (baya) anakufanyia ila kuna vitu vinapinga vilivyopo ndani yako yaweza kuwa ni Mungu au kuna nguvu uliwekewa na wahenga wanaokupenda hasa upande wa pili wa wazazi wako baada ya kung'amua yaliyopo upande wa kwanza, huo ni mtazamo wangu
 
Eeh hatari sana hebu watafute wazee wa ukoo pande zote kwa mama na kwa baba waulize kuhusu hiyo ndoto.
Fanya kwa siri baba ako asijue halafu utakuja kutupa mrejesho.
 
Inakuwaje zaidi ya mara tatu naota napigana na mshua😂, yaani tunapigana sana na mawe wakati mwingine namhurumia lakini na yaye ananitupia mawe inabidi na mimi nimrushie.

Yaani tunapigana sana 😭, ni ndoto ya kujirudia pamoja na kuwa tuna mahusiano mazuri.

Tafsiri tafadhali.

Anayempiga baba na mama yake taa yake itazimika .
 
Kama Una baba yako mtendee mema pia watoto wako hizo sehemu mbili zimebeba Sana baraka .

Kuhusu kugombana ndotoni jaribu kuogea chumvi ya mawe .
 
Back
Top Bottom