Jana jioni niliingia Barbershop nikapaka super black; cha ajabu leo nimeamka kichwani kunawasha sana halafu kumetoka vipele vidogovidogo. Kichwa pia kinauma.. Naomba msaada kwa anayejua tiba ya kutoa hii superb ili niondokane na kadhia nii
Kuna uwezekano ikawa Super black feki. Dawa nyingi za nywele zimeingiliwa pia na wachakachuaji. Cha kufanya osha nywele zako na ondoa hiyo Super black kama bado unayo, au ukiweza nyoa nywele kabisa.
Wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu na dada mmoja ambaye ni mtumiaji wa vipodozi vikali kwa muda mrefu. Alikuwa anatumia CAROTONE lakini sasa anaona ngozi inamuwasha, anakuwa na weusi kuzunguka macho, jua linamuunguza sana na mataizo mengine. Nikampa elimu na ushauri kuhusu CAROTONE na kumuambia kwamba ni kipodozi kibaya na kilichopigwa marufuku hivyo aachane nacho haraka awezavyo. Jibu lake alinishangaza, nikapata hali halisi kwa nini wengi huendelea kutumia. Alinijibu kwamba akiacha ngozi yake inakuwa nyeusi. Pia ulaini wake unapungua na anaona uzuri wa ngozi yake unapotea. Nikamshauri zaidi na kumfariji, kisha tukafikia muafaka baada ya kumsaidia mbadala ambao ni salama na mzuri zaidi kwake.
NILICHOMSHAURI DADA
Nilimshauri dada (Na nawashauri watu wengine wote) aachane na CAROTONE kwa kuwa ni mbaya na tayari inamletea madhara. Hatua ya kwanza ni kuacha kabisa kipodozi hicho ambacho kinakuletea madhara, hata kama kitakuwa kinakuletea matokeo mazuri kiasi gani
Pili kama kimekuletea matatizo ya kiafya ambayo ni ya kutibiwa hospitali basi ni vyema kwenda hospitali kupata ushauri wa daktari na matibabu. Kama ni matatizo ya kutibiwa kwa vipodozi salama basi ni vyema kupata ushauri wa kitaalam na kutumia vipodozi
vilivyo salama ili kuondoa tatizo hilo
Watu wengi hukosea kwa kujaribujaribu vipodozi vingi pamoja na vingine vyenye madhara hivyo kuongeza tatizo. Ukipata madhara kutokana na kipodozi usihangaike tena wala kujaribujaribu, pata ushauri kutoka kwa wataalam wa urembo na vipodozi (Sisi pia tunafanya kazi hiyo) na tumia bidhaa salama.
Tatu kubaliana na hali yako kwa muda wakati unaendelea kushauriwa na kutatua tatizo lako. Kama ngozi itaanza kuwa nyeusi au kutakuwa na baadhi ya chunusi kwa muda basi kuwa mvumilivu wakati unasaidiwa kuondoa madhara ya hivyo vipodozi. Hali hiyo haitadumu na utarejea hali yako ya kawaida na kuishi vizuri, kwa amani.
Nne usirudie tena vipodozi visivyo salama au vile visivyoendana na ngozi yako. Kuwa makini sana na vipodozi, zingatia ubora, usalama na kuendana na ngozi yako na mahitaji yako.
UAMUZI WA DADA
Kutokana na madhara aliyoyapata na ushauri mzuri tuliompa dada alikubali kuacha vipodozi vyote visivyo salama na kufuata ushauri niliompa. Pia alitumia vizuri bidhaa zote nilizomuelekeza na akawa mvumilivu kwa mabadiliko ambayo aliyapata kwa muda mfupi na baada ya siku 10 akawa sawa kabisa.
Nimefurahi sana na kuamua kuwashirikisha katika ushauri na suala hili.
USHAURI KWA WOTE AMBAO WAMEPATA AU WATAPATA MADHARA KUTOKANA NA VIPODOZI
Vipodozi huweza kuleta madhara na matokeo tofauti na yale usiyoyataka wala kuyatarajia. Ikitokea hivyo acha kutumia kipodozi hicho haraka uwezavyo
Kabla ya kutumia kipodozi chochote ni vyema kupata elimu na ushauri mzuri. Pia jua kama kinaendana na ngozi yako na mahitaji yako
Epuka kununua vipodozi ovyo na kuamini watu wasio na utaalam. Pata elimu na ushauri kutoka kwa wataalam na nunua vipodozi kutoka maduka ya vipodozi,
pharmacy na
supermarkets ambako wanauza vipodozi bora na salama tu
Toa taarifa ya kipodozi ulichotumia, mahali uliponunua na madhara uliyoyapata kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA). Hii ni mamlaka ya serikali kwa ajili ya kuratibu na kudhibiti vipodozi na biashara zote za vipodozi Tanzania
Kwa elimu na ushauri zaidi wasiliana na wataalam na washauri wa afya na vipodozi. Ukituchagua sisi karibu sana.