Fafanua mkuu!Karibu Babati tukutoe Lock kwanza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fafanua mkuu!Karibu Babati tukutoe Lock kwanza
Inaweza kuwa shiling ngapi hukoKapange chang'ombe vyumba bei ya dezo na daladala za uhakika hadi mjin kati
Chumba chenye umeme na kumesakafiwa kwa sumendi unapata kwa elfu 15 kwa mwezi na unakula daladala moja hadi town kati. Na in fact hii ndio mitaa yenye daladala za uhakika. Mitaa kama kikuyu, chadulu area A, Area D skuiz haina daladala.Inaweza kuwa shiling ngapi huko
Nashukuru sana Kaka, nitayafanyia kazi mawazo yakoChumba chenye umeme na kumesakafiwa kwa sumendi unapata kwa elfu 15 kwa mwezi na unakula daladala moja hadi town kati. Na in fact hii ndio mitaa yenye daladala za uhakika. Mitaa kama kikuyu, chadulu area A, Area D skuiz haina daladala.
Lakini pia kwa harakaharaka tu afungue pale banda la video aonyeshe "mpira wa ndani" atarudi kusini mihela inamuelemea kuibeba
karibu Mwanza wala hautajutia ujio wakoHeshima kwenu wakuu,
Bila kupoteza muda, Mimi ni kijana wa miaka 27, kwa Sasa nipo kusini mwa nchi lakini siku za usoni natarajia kuhamia Dodoma ili nipambane mbali na nyumbani.
Nimefanya maamuzi haya kwa kuzingatia Mambo mengi:
Kwanza, Dodoma Kuna fursa nyingi za kiuchumi ambazo zimechagizwa na uwepo wa watu wengi (wanafunzi wa vyuo, wabunge, mawaziri na wafanyakazi wengi wa umma). Huku kusini hasa Lindi, kusema ukweli kumesahaulika kabisa, idadi ya watu ni ndogo na mzunguko wa pesa ni mdogo sana.
Pili, Dodoma ni makao makuu ya serikali na ofisi nyingi za umma ziko Dom. Nikiwa hapo sitawaza tena kuhusu interview za utumishi ambapo awali nilikuwa siwezi kuzifanya kutokana na umbali, yaani kutoka huku kwetu hadi Dom kuja kufanya interview ingenighalimu Sana ukizingatia pia interview zinakuwa nyingi kwa post moja (oral na written)
Tatu, ninapafahamu Dodoma kwa uchache, kwasababu nimemaliza degree yangu UDOM, kwaiyo Dodoma ni jiji nalolijua.
Nne, natamani kukaa mbali na home.
Tano, nimepapenda Dodoma.
Changamoto nayoipata (swali nalojiuliza) kwa Sasa ni nini nitafanya nikiwa Dodoma? Na hapa ndio nahitaji mawazo ya wadau na wenyeji wa Dom mnipe faida na hasara, raha na shida za kukaa Dom.
Mwenyewe niliwaza kufanya shughuli hizi,
Kwanza, Bodaboda (kwakua nina kamtaji kidogo naweza nunua pikipiki yangu hata used na Kuanza nayo biashara)
Pili, kuuza nguo na bidhaa nyengine ndogondogo
Tatu, shughuli yeyote ya mtaani Kama kubeba zege, kufyatua matofari n.k.
Kwasasa najipanga ili nisije mikono mitupu katika miji ya watu, nasubiri kidogo nijichange change ili nije vizuri.
Najua huu ni mpango tu na unaweza usiwe sahihi Sana, hivyo nahitaji ushauri wenu wadau, hali ikoje hapo makao makuu? Bei za vyumba vya kupanga ikoje?
Ushauri wenu ni wamuhimu sana, karibuni wanajamiiforums
Asante sanakaribu Mwanza wala hautajutia ujio wako
Hapa ndo atakapojua hajui.Karibu Dodoma
........ila bei ya vyumba vya kupanga ipo juu sana.
Nani kakudanganya?Kapange chang'ombe vyumba bei ya dezo na daladala za uhakika hadi mjin kati
Nashukuru sana, ni ushauri wa kiwango Cha SGRDaaaah! mkuu mimi nilitegemea wakati unasoma chuo UDOM ungekuwa tayari ushafanya utafiti wa kutosha nini utafanya kwenye huo mji wakati utakapomaliza chuo. Tatizo vijana wengi wakiwa chuo hujisahau na kudhani ya kuwa wakimaliza tu chuo watapata ajira.
Binafsi wakati nasoma chuo huko Rock City nilijichanganya sana huko mtaani hasa ziwani, nilizunguka karibu mialo yote ya samaki na dagaa na kufanya tafiti zangu ili kuchek fursa, na nilianza kuchangamkia hizo fursa nikiwa mwaka wa kwanza semester ya pili. Ashukuriwe Mungu sikurudi mkoani kwangu nilipomaliza chuo, nilibaki rock city tena nilihama maeneo ya chuo na kusogea maeneo ya ziwani huko. Nilipiga biashara zangu na sikuwahi kujutia ile biashara maana ilinifanya niishi maisha mazuri tu mjini na sikuwa na ajira.
Ushauri wangu kwako ni huu hapa, tumia network yako uliyoicha huko Dodoma wakati unasoma chuo inaweza kukupa ushauri mzuri wa nini cha kufanya, licha ya hayo network hiyo pia inaweza kukupokea tena mjini na kukupa usaidizi mdogo mdogo hasa wa malazi wakati biashara yako bado changa.
ShukranUkikaribia kuja nichek nikupe room mjini kati bei nzuurii cha kuanzia maishaUmeme na maji vipo
Na mazingira pia yanachangia. Jangwa hilo Mkuu.Dodoma unaweza ukakaa bila kula na watu wanakuangalia tu!! Watu ni wachoyo sana
Kama umeweza kuandika ukafuta, kisha ukaandika tena; basi wewe siyo mvivu Wa kuandika..Sie wavivu wa kuandika tunapata tabu sana, nimeandika nikafuta nikaandika nikafuta.
Sent using Jamii Forums mobile app