Dah... sitaki kuamini km naota au ni kweli, anyways acha nijipe moyo kuwa ni kweli
Ila sasa dada yangu huo uamuzi wa kuamua kukumbatiwa na mtu anaekuzidi pesa mbona naona si mzuri!!!!!!!
Pesa huwa inatafutwa tu huwezi kujua huyo unaemwacha kesho atakua nani. Kwani nani alijua km wewe leo ungekua na cheo na mshaara mzuri kuliko huyo bf wako wa sasa? naamini km wewe ungejua hivo basi usingekua nae. Vp ukiachana nae halafu mambo yake yakawa mazuri baada ya muda kidogo? samahani sikuombei mabaya lakini ebu naomba ufikirie km ikitokea kwa bahati mbaya tu (samahani sio lengo langu) mshahara huo ukapungua au ukaachishwa kazi mambo yatakuwaje?
kuna uzi niliusoma hapa kuhusu dada wa sua aliyemwacha mnyarwanda na kuolewa na college mate wake baadae mnyarwanda akabahatika kuwa waziri, dada amebakia kujuta. Nakushauri ukae chini ufikirie kuhusu huo uamuzi wako please,
I am sure kwa uamuzi huo ipo siku utajuta tu japo hutasema lakini ipo siku utakumbuka haya nisemayo
Nakutakia kila la heri
Thanks