Nimepata kidonda kikubwa kwenye kichwa cha uume baada ya kunywa malafin

Nimepata kidonda kikubwa kwenye kichwa cha uume baada ya kunywa malafin

Mkuu, pole sana. Dawa uliyotumia huwa na mjumuiko wa kemikali ya sulfa ambayo kwa baadhi ya watu husababisha allergy (mzio) kubwa au ndogo.

Hii ni ishara ya kuwa mwili wako hauna ustahimilivu kwa sulfa, hivyo jaribu kutumia dawa zingine kwa kadri mwongozo wa Serikali unaohusisha matibabu ya ugonjwa huu unavyosema.

JamiiForums kupitia jukwaa lao la Jamii Check wameelezea suala hili kwa undani, unaweza kusoma hapa: Baadhi ya Dawa za kutibu Malaria zinaweza kusababisha mzio mwilini, ikiwemo Kuchubuka Uume na Midomo
Asante mkuu kwa uzi nimeutazama.
. Naweza kausha hiki kidonda kwa dawa gani?
 
Asante mkuu kwa uzi nimeutazama.
. Naweza kausha hiki kidonda kwa dawa gani?
Napata kigugumizi kushauri moja kwa moja hoja yako mkuu kwa kuwa sijui ukubwa wa madhara yaliyotokeza haaa ikihusisha ukubwa wa hicho kidonda pamoja na matazamio ya uponaji wake.

Lakini, kitu pekee ninachoweza kushauri ni kuwa sitisha matumizi ya hiyo dawa, kisha fika hospitalini wakubadilishie. Kwa kuwa utakuwa hapo, wao watapata wasaa wa kukuchunguza kwa ukaribu.

Ushauri muhimu zaidi kwako, uwe makini na dawa zenye kemikali hii. Kila dawa unayonunua kwa sasa jiridhishe kwanza kama haina kemikali hizo, maana zipo kwenye dawa nyingi ukiondoa hizo ulizopatiwa.
 
Dah! Hi hali ilinisumbua sana kabla sijagundua tatizo. Uume ulipata kidonda siku moja mara tu baada ya kumeza hizo dawa.

hizo malafin zina sulfur ambayo baadhi yetu tuna allergy nayo.
 
Isije ikawa Kaswende/Herpes maana huwa inachukua muda ndipo ijiyokeze.
Unawza ukasex leo then baada ya Wiki/mwez kutegemeana na kingabya mwili wako vikajitokeza hivyo Vipele

Pole sana Mwamba Mlafin ukiisoma Side Effect haionyesh kuleta vidonda kwenye Uume yan Not Revommended to such effect

Kindly go Hospital for STDs checkup
Samahan lkn sijakushtumu
 
Dah! Hi hali ilinisumbua sana kabla sijagundua tatizo. Uume ulipata kidonda siku moja mara tu baada ya kumeza hizo dawa.

hizo malafin zina sulfur ambayo baadhi yetu tuna allergy nayo.
Ulikausha vipi kidonda au kilipona chenyewe?
 
Napata kigugumizi kushauri moja kwa moja hoja yako mkuu kwa kuwa sijui ukubwa wa madhara yaliyotokeza haaa ikihusisha ukubwa wa hicho kidonda pamoja na matazamio ya uponaji wake.

Lakini, kitu pekee ninachoweza kushauri ni kuwa sitisha matumizi ya hiyo dawa, kisha fika hospitalini wakubadilishie. Kwa kuwa utakuwa hapo, wao watapata wasaa wa kukuchunguza kwa ukaribu.

Ushauri muhimu zaidi kwako, uwe makini na dawa zenye kemikali hii. Kila dawa unayonunua kwa sasa jiridhishe kwanza kama haina kemikali hizo, maana zipo kwenye dawa nyingi ukiondoa hizo ulizopatiwa.
Sawa mkuu nimekuelewa. Hata hivyo dawa nilikunywa single dose hivyo sitegemei kuzitumia tena.

Kuhusu kidonda ni kibichi kinamelemeta mafuta. Nilitaka kwanza nipone hiki kidonda maana ni mtihani kufanya shughuli zangu.
 
Sawa nitakutumia picha Pm roho yako itulie.
Unadhani ukienda hosp hutaulizwa uoneshe? Au sababu humu ndani hatujuani na hatuandiki kama ni matabibu mnatuchukulia poa? Kidonda lazima kiangaliwa kionekane kikoje then ndo ushauriwe.
 
Back
Top Bottom