Nimepata maumivu makali mno baada ya Ufaransa kushindwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la dunia 2022

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Yaani nashindwa nielezee vipi ili nieleweke.

Jana baada ya fainali ya kombe la dunia kumalizika nilipata maumivu makali sana ambayo sijawahi kuyapata kwenye masuala ya kimichezo yaani moyo ulikuwa unauma sana alafu nikawa sina raha kabisa. Nilijishangaa sana kutokana na hiyo hali, kwakwel niliumia sana na nikanyongonyea mithili ya mrenda.

Nilipenda sana Ufaransa atwae huo ubingwa lakini haikuwa hivyo, ilifika kipindi ukitizama kikosi cha Ufaransa chote ni Waafrika kasoro kipa wao tu, nilipenda sana hao wabaruya wachukue ubingwa. Pongezi sana kwa Mbappe

Mpaka sasa hivi bado nina maumivu makali sana, nimejaribu kutumia dawa za kutuliza maumivu lakini bado sijapata nafuu yoyote ile. Poor me
 
pole sana, maumivu kama hayo aliyapata messi miaka 8 iliyopita. mjinadae na 2026 bado mna vijana wadogo watakuwa matured vya kutosha kupambana zaid by hyo 2026
 
Messi ni ugonjwa usiotibika jitahidi umkubali hata kishingo upande, itakusaidia kupunguza machungu.
 
Hiki kiumbe nakikubali sana aisee hanaga makuu
Napendaga watu wa aina hii
 
Nadhan ukienda chooni inaweza kukusaidia
 
Tatizo vijana mnabett
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…