Nimepata Msiba WanaJF

Nimepata Msiba WanaJF

Ngugu yangu Sipo,
Pole sana kwa msiba mzito kuondokewa na Babu ambaye alichuku nafasi nzito katika malezi yako kama ulivyoeleza. Nakuombea Mungu azidi kukupa nguvu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.
 
Pole sana Sipo, Inna lillahi wa inaa illahi rajiun....to Allah we belong and to Him is our retunrn. Nakuombea wewe na familia subira katika wakati huu mgumu.
 
Jamani jinsi ya kumchangia mwenzetu katika hili
naomba atusaidie hata kama ni ngumu kumpata basi tumtumie hata vijidola vya tigo,voda kwa mawasiliano....mungu akupe roho ya uvumilivu mpwa...mungu awafikishe salama kama mnasafirisha
 
Pole sana, Mungu akupe ujasiri na utulivu kwenye kipindi hiki kigumu kwako.
+ R.I.P mpendwa wa Sipo.
 
Pole sana Ndugu yangu,Mwenyezi mungu akupe Nguvu na Ujasiri katika kipindi hichi kigumu cha Msiba.Mwenyezi Mungu amlaze Mahali Pema Peponi Mpendwa Babu yetu.Ndg Sipo tupo pamoja katika sala za kumuombea babu!
 
Pole sana rafiki yangu SIpo

Mshukuru mungu zaidi kwa kumpa uhai babu na kukupa wewe uhai mpaka ukamfahamu.

Mungu amekuonyesha thamani ya uzee na wewe basi ichukue uienzi!!

Tusherehekee maisha ya babu kwa kuenzi mema ya senior citizens wetu

Kila nafsi itaonja mauti!!
 
Pole kwa msiba mzito! Mungu na akupe nguvu kuweza kustahimili wakati huu mgumu
 
Pole sana ndugu, Mwenyezi Mungu Insha'Allah akujaalie subra na uvumilivu, kipindi hiki cha msiba.
 
Pole sana ndugu..Mwenyezi mungu akupe subira ..wote tunatoka kwake na marejeo ni kwake..
 
Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. Amen

msiba mzito.

...Babu ametangulia nasi tutafuatia...njia ya sote hiyo.
Pole sana Sipo,

...mw'mungu azidi kukupa nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Poleni sana.
 
Pole sana mkuu, na mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi.
 
Mkuu Sipo pole sana kwa msiba mkubwa uliokufika wewe, ndugu, jamaa na marafiki. Namuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja kipindi hiki kigumu kwenu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN
 
Pole Sana Sipo. Muumba Amrehemu Na Kuiweka Roho Yake Pahala Pema Peponi. Amina.

SteveD.
 
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe. Pole sana swahiba. Tuko pamoja. R.I.P Babu yetu.
 
Back
Top Bottom