Habari zenu wadau? mimi mzima
Nimebahatika kupata msichana mkali ambaye hata mimi kuna wakati naona alinionea huruma tu kuwa na mimi.
Huyu msichana ana tabia moja ya ajabu ambayo hata mimi napata wakati mgumu kuielewa,yaani ana tabia za kiume balaa kuna wakati na mfananisha na
Kasinde (no hard feelings), kuanzia kuongea,kutembea,mavazi,aina ya muziki anaosikiliza,marafiki,maongezi na kila kitu.
Lakini juzi ndipo nilipochoka baada ya kumuuliza yuko wapi akanijibu yuko Mwenge Meridian,ameenda kubeti mechi ya Arsenal na Tottenham