Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Ni muda sasa niko naye. Ananiamini fika, na istoshe kashanijulisha michongo ya hapa na pale ambayo humuingizia kipato. Siku nyingine hunialika ofisini kwake, natulia pale asubuhi mpaka jioni. Gharama za chakula na vitu vidogo vidogo ni juu yake japokuwa huwa sipendi kutawaliwa na mwanamke especially financially, nimejikuta tu sina usemi kwa huyu binti. She's so smart na ninaamini ananipenda kutoka moyoni. Muda mwingine niwapo kazini kwake, may be nikaenda short call, ninaporudi tu nakuta pesa imezidi kwenye wallet.
Vizawadi kama vile t-shirts, viatu, cadets vyote hivyo nimejaza ndani.
Siku ya jana asubuhi ilikuwa ni siku ya yeye kwenda kunitambulisha kazini kwa mama yake ili nami nipate kumfahamu. Hii ni baada ya mama yake kumsistiza niende anifahamu. Binti anaeleza sababu ni kuwa mama yake ameguswa na the way mahusiano yake yamekuwa serious kiasi cha kuwa reflected kwenye maisha ya binti ya kila siku.
Tulifika somewhere karibu na mashine ya kuchakata unga wa sembe. Ni brand kubwa tu niliyoiona kwenye zile mifuko ya kupakilia, ni maarufu. Binti akanitaka nikae kwenye kiti cha plastic pale nje, ambapo mbele yangu kulikuwa na gari jeusi lenye kupendeza lenye usajili wa ***
Nilipata wasaa wa kumuuliza binti kuwa kazini kwa mama yake ndio hapa? Akanambia sio, ila hapa tunapumzika tu. Binti akawa ametoka kidogo!
Dakika si nyingi, muda ambao kausingizi kananipitia hivi nilishtushwa na mama muongeaji mnene, kavaa miwani transparent na minywele mingi ya njano huku mkononi kashilia tambo haswa! Kwenye bega kunaning'inia mkoba wa thamani, kavaa vazi la kitenge. Alikuwa na mwenzake mwembamba tu. Baada ya kufika pale alianza kukaripia huku akilaumu kuwa kuna kiroba chake kiliegeshwa kwenye gari kilikuwa na mahindi kiko wapi!
Huku akifoka kuwa mimi niliekuwa pale ndiye niliekibeba! "Hawa vijana wa mtaani wanaokaa hapa wengi wao ni vibaka, atanieleza leo kiroba changu kapeleka wapi!" Baada ya kesi kusuluhishwa, nilisogea kwa mbele kidogo na kusimama. Binti alifika mbele yangu na kuniuliza kuwa "mbona nilikokuacha sijakukuta?" Nikaamua kumuongopea!
Akanambia tumsubiri mama yake anakuja. Baada ya muda nikaona lile gari jeusi lenye namba za usajili *** likisogea mbele yetu, kisha kioo kufunguliwa, nikaona sura ya yuleyule mama ikitutazama kwa mshangao...
Nitaendelea baadae kidogo...