Nimepata pigo naomba ushauri

Nimepata pigo naomba ushauri

Cameo

Member
Joined
Jul 22, 2015
Posts
5
Reaction score
1
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 20 nilimaliza form four 2013 namshukuru mungu nilifaulu na kupata division one.
Nilipokuwa naanza form 5 quarter ya kwanza shuleni nilisumbuliwa na magonjwa fulani ambayo yaliniweka nje muda mrefu na ikabidi nipostpone mwaka wa masomo ili nipate matibabu kikamilifu hivyo mwezi huu wa saba ndio inabidi niaanze upya form 5...
Sasa tatizo langu ni kwamba napata depression kuona wenzangu wameniacha pia kwenda kusoma na watoto ambao nimewazidi miaka 2-3, pia napata mashaka kuona ntamaliza chuo na umri mkubwa wa miaka 25 ukilinganisha na wengine watamaliza na 22-23, naomba ushauri tafadhali!!!
 
Nenda kasome diploma au certificate huko ndo wakubwa wemzako wapo
 
Mimj nasima chuo na wanangu,sembuse wewe.kama hutaki acha kachome mkaa uchindile uone timbwili timbwili lake kama la asha ngedere hivi
 
Anyway.Bwana mudogo usiishi kwa kuangalia watu ishi kwa kujiamini. Wewe kama Wewe. Usiruhusu kabisa kufanya jambo kwa kuwaridhisha watu.Do what is best for you before its too late.Kupitwa na rika lako sio ishu.Ishu ni kupata kitu sahihi bila kujali wakati gani.
 
Anyway.Bwana mudogo usiishi kwa kuangalia watu ishi kwa kujiamini. Wewe kama Wewe. Usiruhusu kabisa kufanya jambo kwa kuwadhirisha watu.Do what is best for you before its too late.Kupitwa na rika lako sio ishu.Ishu ni kupata kitu sahihi bila kujali wakati gani.

Asante mkuu kwa ushauri wako ntautendea kazi
 
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 20 nilimaliza form four 2013 namshukuru mungu nilifaulu na kupata division one.
Nilipokuwa naanza form 5 quarter ya kwanza shuleni nilisumbuliwa na magonjwa fulani ambayo yaliniweka nje muda mrefu na ikabidi nipostpone mwaka wa masomo ili nipate matibabu kikamilifu hivyo mwezi huu wa saba ndio inabidi niaanze upya form 5...
Sasa tatizo langu ni kwamba napata depression kuona wenzangu wameniacha pia kwenda kusoma na watoto ambao nimewazidi miaka 2-3, pia napata mashaka kuona ntamaliza chuo na umri mkubwa wa miaka 25 ukilinganisha na wengine watamaliza na 22-23, naomba ushauri tafadhali!!!
Rudi chekechea hao wazuri zaidi
 
wenzako tumemaliza chuo na umri mdogo.
tunaishia kuzeeka mtaan..
Maisha hayana fomura we kazana upite njia sahihi...
 
mwalimu wangu aliyenifundisha elimu ya msingi tena darasa la tano.. ALINIKUTA CHUO KIKUU MIMI NIKIWA MWAKA WA TATU YEYE NDIO ANAINGIA WA KWANZA. mwingine tulienda nae sawa..wangekuwa na akili kama zako wasingesoma ..
 
daa umri tu ndio unaona tatizo? vip kuhusu kuharibu future yako? think twice.
 
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 20 nilimaliza form four 2013 namshukuru mungu nilifaulu na kupata division one.
Nilipokuwa naanza form 5 quarter ya kwanza shuleni nilisumbuliwa na magonjwa fulani ambayo yaliniweka nje muda mrefu na ikabidi nipostpone mwaka wa masomo ili nipate matibabu kikamilifu hivyo mwezi huu wa saba ndio inabidi niaanze upya form 5...
Sasa tatizo langu ni kwamba napata depression kuona wenzangu wameniacha pia kwenda kusoma na watoto ambao nimewazidi miaka 2-3, pia napata mashaka kuona ntamaliza chuo na umri mkubwa wa miaka 25 ukilinganisha na wengine watamaliza na 22-23, naomba ushauri tafadhali!!!

kwanza kwa nini hupati depression wenzako wagonjwa walikufa wewe uko hai? , wenzako walomaliza f4 wana zero hawategemei kumaliza chuo maishani hata wawe na miaka 69? aliyekwambia miaka25 ni mingi kwakumaliza chuo nani?

mshukuru mungu ulifaulu &umepona na unaendelea na shule mdogo wangu mpendwa. soma kwa bidii huo umri usikutishe kwanu hao watoto kuna waloficha umri wai waliresit mara kibai hapo utakuta ni kaka zako na dada zako.

cha msingi piga kitabu ufaulu vizur hapo wewe ndo utakuwa babyy .

usipende kufanya mambo kwakuangalia watu hutakaa ufanikiwe, ukifika chuo utashangaa kukuta watu wana miaja 40 ndo kwanza wanasoma chuo mara ya kwanza.
kila la kheri usome kwa aman na ufaulu
 
Soma acha mawazo ya kitoto wewe.

Kweli huyo aache utoto mbona me pia nimepata hayo matatizo lakini nakaza, kuna watu wanamaliza mpaka na miaka 28-30 lakini wanakaza elimu haina mwisho... Akifikisha miaka 40 atajishangaa sana wasiwasi alionao now, na pia achague kufika 20 year with or without education sababu apende asipende umri utafika tu..
 
Back
Top Bottom