Nimepata wazo la kufanya Biashara ya mazao ya chakula (mchele,mahindi,unga,maharage)

Nimepata wazo la kufanya Biashara ya mazao ya chakula (mchele,mahindi,unga,maharage)

Joined
Jan 16, 2025
Posts
1
Reaction score
2
Habari wana jamii
Kwa jina naitwa Juma Issa Mikidadi, ni kijana mwenye shahuku ya maendeleo . Nimepata wazo la kufanya biashara ya mazao ya chakula yaan mchele, maharage , mahindi na unga. Eneo ni Mtwara .

MALENGO:
1:Nitakuwa naenda kununua moja kwa moja kwa wakulima au kwenye masoko ya jumla
2:Nitafungua stoo ambapo nitakuwa nauza either kwa jumla au rejareja.
3:nitakuwa nafanya online business kwa wale wateja ambao wapo mtandaoni na wanawish kuweka oda na kufanyiwa deliverly ndani ya Mtwara mjini.
4:Nitafanya direct sales kwa kupita kwenye maduka na kuwatangazia bidhaa zangu .
5.Nitafanya credit sales kwa wateja wa uhakika mfano wa super market, min market, hotels and restaurant.
6:Nitafaya free deliverly ndani ya wilaya kwa wateja kutokana na mzigo utakaochukua.
7:Nitafungua website, na social networks pages and accounts kwa ajiri ya matangazo ya biashara.
8:nitakuwa nachunguza fursa zilizopo kwa wakulima kipindi nanunua mazao mfano kam kuna soko la mbolea na mbegu basi nitawaletea na kuwauzia.

MAOMBI KWA WANAJAMII
1:Kama kun chochote unaweza nishaurii naweza kufanya ili kupata faida juu ya biashara hii
2:Changamoto zozote ambazo zipo kwenye biashara hii
3:sehemu ambazo naweza pata mazao hayo kwa bei rahisi au kama una mtu unamjua anauza kwa jumla
4:Sehemu zipi kwa songea naweza pata maharage , mahindi,na mchele kwa bei rahisi
5:Wapi naweza pata usafiri na gharama za kusafirisha mzigo kutoka songea hadi Mtwara

Asanteni
 
Uzi wako umekaa poa.. nadhani wenyeji wa hii mikoa wanaweza kua na lolote la kushaurii..
 
 
1738564139756logo.jpg.png

Mawazo 114 ya Biashara na Mitaji yake: Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuanzisha Biashara 114.
Whatsapp: 0687746471
 
Back
Top Bottom