Nimepata wito wa Mahakama, naombeni msaada!

Bosco Ntaganda

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
710
Reaction score
289
Habari ndugu zangu?

Jana nimepokea wito wa kwenda mahakamani bila kukosa. Kuna taasisi ina nidai, sasa imekosa uvumilivu na kuamua kunibuluza mahakani!

Kwasasa hiyo pesa ya kuwalipa haipo, je nikifika mahakamani naweza kujitetea vipi?

Nikubali kosa ama nikatae ili kesi ihahilishe? Au nikubali kosa itolewe hukumu?

Wataalamu wa kesi za madai, Tafadhali naombeni ushauri wenu.
 
Deni halifungi. Kubali, waambie utakuwa polepole. Huo ndo uwezo wako
 
Dawa ya deni kulipa.....

Hehehe, kiongozi sijakataa kulipa, ila hiyo pesa kwasasa haipo. Jamaa wanadai zaidi ya milioni 50!
Nafasi yangu ya kulipa ni hadi mwezi Julai katikati. Vipi naweza kujitetea namna gani mahakamani?
 
inategemea wamefungia kesi gani mkuu...
 
Inategemea mkuu iyo charge imefunguliwaje halo ndipo utajua ukane au ukubali.Ila Mara nyingi hizo kesi no breach of contract
 
Deni halifungi. Kubali, waambie utakuwa polepole. Huo ndo uwezo wako
Shukrani kwa ushauri kiongozi. Vipi, mahakama inaweza kukubali kunipa muda ninaotaka mimi? Yaani wanaweza kukubali muda nitakao kuwa tayari kuanza kulipa?
 
Inategemea mkuu iyo charge imefunguliwaje halo ndipo utajua ukane au ukubali.Ila Mara nyingi hizo kesi no breach of contract

Sijakuelewa kiongozi! No breach of contract?
Nikweli niliamua kuvunja mkataba na kuwaambia nitawarudishia pesa yao, sasa wamekosa uvumilivu na kuamua kunipeleka mahakamani, wakitaka pesa yao ilejeshwe mara moja.
 
inategemea wamefungia kesi gani mkuu...

Wamefungua kesi ya madai kiongozi, wanataka mahakama iniamuru kuwalipa pesa yao mara moja!
Nikifika mahakamani nikubali ama nikatae kosa? Matokeo yake yatakuaje?
Na je, mahakama inaweza kukubaliana na mimi kuhusu muda wa kulipa hilo deni iwapo nitakubali ?
 
Sijakuelewa kiongozi! No breach of contract?
Nikweli niliamua kuvunja mkataba na kuwaambia nitawarudishia pesa yao, sasa wamekosa uvumilivu na kuamua kunipeleka mahakamani, wakitaka pesa yao ilejeshwe mara moja.

breach of contact iko kiupana wake nipm nitakupa namna ya kushinda wanahangaika tu
 
breach of contact iko kiupana wake nipm nitakupa namna ya kushinda wanahangaika tu

Sawa kiongozi nakucheki sasahivi. Jambo lingine linaloniumiza kichwa, ni kwamba kwasasa niko nje ya mkoa husika, kwa kazi fulani hivi. Kwa vyovyote vile sitaweza kuhudhuri mahakamani katika siku husika, nini hatima yangu hapo?
 
POA haina shida
 
Deni halifungi. Kubali, waambie utakuwa polepole. Huo ndo uwezo wako

Mahakama inaweza kukubali nianze kulipa muda nitakao kuwa tayari? Na nisipoweza kuhudhuria huo wito(kutokana na kuwa mbali na eneo la tukio, kwa kazi maalum), itakuaje kwa upande wangu?
 
Huna haja ya kupoteza mda na kujiongezea garama bure, wewe kubali halafu omba mda ulipe
 
Hao wenyewe mkuu inaonyesha sio wapenda kesi' wangekua wapenda kesi wangekua wameshakushindilia na hati ya madai (plaint) saa hizi unatafuta hela ya wakili akujibie. Hao wa wito!!! Sio watu wa kesi unaweza cheza nao vizuri tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…