Nimependa wazo la kijiji cha Mundindi kununua hati fungani, wameweza ndoto iliyowashinda Simba SC

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kijiji cha Mundindi kilichopo wilayani Ludewa kilipewa fidia ya Tshs 464 na kati ya hizo Tshs 400 milioni waliamua kununua hati fungani katika benki mojawapo nchini itayowapa gawio la Tshs 41 kila mwaka. Kijiji kilipata fedha hizo baada ya kupewa fidia ya ardhi kutoka Serikalini baada ya kupisha mradi wa Liganga na Mchuchuma, kijiji kilikuwa na eneo. Jumla Serikali ililipa fidia ya bilioni 15.

Mohammed Dewji wakati anapiga chapuo la kununua hisa za Simba alikuwa na ndoto hizi pia, kwamba zile bilioni zake 20 akanunulie hati fungani na gawio la kila mwaka litumike kuendesha klabu lakini baadae wakadai wametumia mtaji kuendesha klabu. Lilikuwa jambo jema kwasababu timu ingekuwa na mtaji endelevu.

Natoa rai kwa wanakijiji wa Mundindi wawe wafuatiliaji wasije kuingia wajanja kati na kuwakwapulia dira yao njema, pia sehemu gawio waendelee kuongeza kiwango cha fungani walizonazo kwani shilingi yetu ina kasi nzuri ya kushuka. Serikali wasitumie gawio la wanakijiji kama fimbo ya kutopeleka fedha wakiamini watajiongeza kwenye fedha za gawio.

Wanakijiji_Mundindi.jpeg

Wanakijiji wa Mundindi wilayani Ludewa​
 
View attachment 3042729
Wanakijiji wa Mundindi wilayani Ludewa​
wanavaa kiheshima sana
 
Nimesoma sehemu ikielezea kwamba pesa nyingine zilitumika kukatia kila mwanakijiji Bima ya Afya
 
Tanganyika itajengwa na watu wenye Moyo safi na waaminifu.
viongozi kama hawa niwachache sana kwa sasa na tumewapoteza kwa mlo wetu wa siku moja tukatumia kura kuwaangamiza.
hongera sana
 
Back
Top Bottom