Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 422
- 893
Poleni na majukumu,
Umri wangu ni miaka 32, hapo nyuma nikiwa na miaka 27 nilibahatika kuwa na mahusiano na mwanamke anayenizidi umri kwa miaka 7,ana mtoto mmoja ana kazi yake hivyo alikuwa akinipa vihela vidogovidogo na ndicho nilichompendea.
Nilipofika miaka 28 nikaanza kupata ushawishi wa kuoa kutoka kwa wazazi wangu, kwa kuwa nilikuwa nampenda huyo mwanamke niliwaeleza kila kitu kumuhusu.
Wakashauri nitafute mwanamke ambaye ni mdogo kwangu hata kama ananizidi isizidi miaka 2. Nami nikaanza kutafuta polepole nikampata ninayemzidi umri na miaka 30 nikaoa, sasa nina mtoto mmoja na mke wangu. Vitu vyote hivi nilifanya bila kumshirikisha mpenzi wangu mpaka nafunga ndoa kwa sababu nilijua nikimwambia ataumia sana alikuwa ananipenda mno.
Siku ya Harusi nilipost picha mtandaoni akaziona (Tunaishi mikoa tofauti) kwa kweli aliumia sana, baada ya siku kadhaa akaniambia hata kama nilikuwa simtaki ningemwambia yeye asingenikataza kuoa mke ninayemtaka alilia sana kwenye simu.
Sasa ananilaumu nimemharibia future yake alikuwa anawakataa wanaume kwa ajili yangu. Alikuwa na mpango wa kuongeza watoto alikuwa amesubiri nimuoe ili azae nami.
Anataka nimuoe awe mke wa pili hata kama kwa siri mke wangu asijue. Anasema hawezi kuishi bila mimi, nifanyaje naombeni ushauri wenu.