Nimependwa na mwanamke mtu mzima, naomba ushauri

Nimependwa na mwanamke mtu mzima, naomba ushauri

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Poleni na majukumu,

Umri wangu ni miaka 32, hapo nyuma nikiwa na miaka 27 nilibahatika kuwa na mahusiano na mwanamke anayenizidi umri kwa miaka 7,ana mtoto mmoja ana kazi yake hivyo alikuwa akinipa vihela vidogovidogo na ndicho nilichompendea.

Nilipofika miaka 28 nikaanza kupata ushawishi wa kuoa kutoka kwa wazazi wangu, kwa kuwa nilikuwa nampenda huyo mwanamke niliwaeleza kila kitu kumuhusu.

Wakashauri nitafute mwanamke ambaye ni mdogo kwangu hata kama ananizidi isizidi miaka 2. Nami nikaanza kutafuta polepole nikampata ninayemzidi umri na miaka 30 nikaoa, sasa nina mtoto mmoja na mke wangu. Vitu vyote hivi nilifanya bila kumshirikisha mpenzi wangu mpaka nafunga ndoa kwa sababu nilijua nikimwambia ataumia sana alikuwa ananipenda mno.

Siku ya Harusi nilipost picha mtandaoni akaziona (Tunaishi mikoa tofauti) kwa kweli aliumia sana, baada ya siku kadhaa akaniambia hata kama nilikuwa simtaki ningemwambia yeye asingenikataza kuoa mke ninayemtaka alilia sana kwenye simu.

Sasa ananilaumu nimemharibia future yake alikuwa anawakataa wanaume kwa ajili yangu. Alikuwa na mpango wa kuongeza watoto alikuwa amesubiri nimuoe ili azae nami.

Anataka nimuoe awe mke wa pili hata kama kwa siri mke wangu asijue. Anasema hawezi kuishi bila mimi, nifanyaje naombeni ushauri wenu.
 
Vijana wa siku hizi bwana,sjui mkoje !anyway muoe tu!

Lakn kumbuka,asiyeskia la mkuu,huvunjika guu
 
Umependwa na shangazi kwani wewe humpendi jishangazi ilo kama unampenda kwanini hukumuoa? Kama humpendi muache kuepuka lawama badae
 
Poleni na majukumu,
Umri wangu ni miaka 32, hapo nyuma nikiwa na miaka 27 nilibahatika kuwa na mahusiano na mwanamke anayenizidi umri kwa miaka 7,ana mtoto mmoja ana kazi yake hivyo alikuwa akinipa vihela vidogovidogo na ndicho nilichompendea.
Peleka moto mpelekee moto
 
32 + 7 = 39 this is dusk moment
Poleni na majukumu,
Umri wangu ni miaka 32, hapo nyuma nikiwa na miaka 27 nilibahatika kuwa na mahusiano na mwanamke anayenizidi umri kwa miaka 7,ana mtoto mmoja ana kazi yake hivyo alikuwa akinipa vihela vidogovidogo na ndicho nilichompendea.
 
Kwa wale wavivu ngoja niwape summary:

Ana miaka 32, ameoa kwa maelekezo ya wazazi huku akiwa anatembea na jimama, alipenda jimama sababu linampa vipesa vya hapa na pale.

Anaomba ashauriwe kuhusu hilo jimama sababu bila kuwa nalo jimama linasema litafariki.
 
Ahaaahaaahaa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
DJ mlete mke wa pili!!
Mi napita zangu ukioa leta mrejesho
 
Back
Top Bottom