nimepewa barua ya kufika mahkamani kwa kushindwa kulipa pesa ya taka

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
765
Reaction score
490
Habari zenu waheshimiwa wanasheria , kiukweli mm nimepata hii barua na nimeambia wakufika mahkamani kwa kushindwa kulipa pesa ya taka, hii imekuja baada ya habari ifuatayo

mm nina kijifremu ambacho ukubwa wake ni kama kabati la tano kwa sita la nguo hapo kariakoo msimbazi na agrey na nashungulika na biashara ya simu na kwa siku nauza simu tano mpaka 10 ambapo taka ninazo zizaliasha hata kwenye kisado kidogo hakijai kwa siku
Hapo mwanza kabla ya mwezi wa sita mwaka 2012 nilikua nalipa pesa ya taka kwa kampuni ya moto investment kwa shilingi elfu kumi (10,000) kwa kila mwezi na nililipa miezi yote ya huko nyuma bila ulalamishi wowote ila cha kushangaza ghafla mabwana hawa wa moto investment wakapandisha gharama za uzoaji taka kwa kila fremu kutoka elfu kumi(10,000) mpaka elfu sitini (60,000) kwa mwezi kwa kila fremu tukaenda kwa afsa mtendaji ili kuomba watupunguzie bei wakadai wao hawawezi kushughulikia suala hili ,nikaenda serikali za mitaa wakadai wao hawawezi kushugulikia suala hili kila sehemu ninazoenda wananirusha rusha mpaka juzi tarehe 5 wakaniletea barua ya kuniita mahkama kwa kutolipa pesa ya taka nyinyi wanasheria mnanisaidiaje mm sheria siijui hata siku moja wala huko kituo cha polisi sikuwahi hata kufika!
 
kweli nchi inaliwa na wenye meno, elfu 60,000?????????????? wanatumia vigezo gani kuamua huyu alipe elfu sitini huyu ngapi? Mbona kkoo kwenyewe kuchafu sana tu???? Au kuna 10% za watu? hivi JERRY slaa hayupo humu atujibu? Si wilaya yake hiyo????
 
Last edited by a moderator:
Dah!! Wezi wa meno ya tembo, ndege ya laki 5 mbona hawapewi barua za kwenda mahakamani ?

Sent via EyePhone
 
Usiogope nenda mahakani usikie wanakuambia nini then njoo uje utupe walichokuambia tutakushauri vizuri ikiwa na nisheria ipi inayokushtaki na mabadiliko ya iyo sheria kutoka elfu kumi kwenda elfu sitini sawa mkuu
 
Ambatanisha stakabadhi za malipo ya awali kisha nenda navyo mahakamani.
 
Habari zenu waheshimiwa wanasheria , kiukweli mm nimepata hii barua na nimeambia wakufika mahkamani kwa kushindwa kulipa pesa ya taka, hii imekuja baada ya habari ifuatayo

mm nina kijifremu ambacho ukubwa wake ni kama kabati la tano kwa sita la nguo hapo kariakoo msimbazi na agrey na nashungulika na biashara ya simu na kwa siku nauza simu tano mpaka 10 ambapo taka ninazo zizaliasha hata kwenye kisado kidogo hakijai kwa siku
Hapo mwanza kabla ya mwezi wa sita mwaka 2012 nilikua nalipa pesa ya taka kwa kampuni ya moto investment kwa shilingi elfu kumi (10,000) kwa kila mwezi na nililipa miezi yote ya huko nyuma bila ulalamishi wowote ila cha kushangaza ghafla mabwana hawa wa moto investment wakapandisha gharama za uzoaji taka kwa kila fremu kutoka elfu kumi(10,000) mpaka elfu sitini (60,000) kwa mwezi kwa kila fremu tukaenda kwa afsa mtendaji ili kuomba watupunguzie bei wakadai wao hawawezi kushughulikia suala hili ,nikaenda serikali za mitaa wakadai wao hawawezi kushugulikia suala hili kila sehemu ninazoenda wananirusha rusha mpaka juzi tarehe 5 wakaniletea barua ya kuniita mahkama kwa kutolipa pesa ya taka nyinyi wanasheria mnanisaidiaje mm sheria siijui hata siku moja wala huko kituo cha polisi sikuwahi hata kufika!

walio kushitaki ni kampuni au serikali ya mtaa?
 
walio kushitaki ni kampuni au serikali ya mtaa??
 
Ambatanisha stakabadhi za malipo ya awali kisha nenda navyo mahakamani.

mkuu unapoishia kwa kumshauri aambatanishe stakabadhi na barua kisha aende mahakamani, it means aende kupigwa navyo picha au?? Si bora tu hata ungemshauri amsalimie hakimu akienda mahakamani?
Toa msaada kama unaweza, kama huwezi unaacha.
 
Gharama za kuzoa taka kupanda kutoka 10,000 mpaka 60,000? That's a 6005 increase. Kisa?

Na kwa nini mtu uandamwe kwa kukataa kushiriki huo mfumo wa uzoaji taka? Ukitaka kuzoa taka zako mwenyewe je? Yaani wanalazimisha hata kama unaweza kuzoa taka zako mwenyewe kwa gharama nafuu usizoe?

Sehemu yako ina uchafu? Una hakika hiyo barua imetoka mahakamani?
 
Hizo tenda mara nyingi zinatolewa na Manispaa kwahiyo kampuni hutoa bid kwa kuonesha kiasi itakacho kusanya na kisha kuilipa manispaa kwa mujibu wa makubaliano lakini ni ajabu kwa fee kutoka 10 mpka 60 hii si kawaida.. wewe nenda mahakamani ukaskilize wito wako then ukirudi hapa tujuze hicho kipya tunaweza tukawa na ushauri mzuri zaidi
 
Hao kina jeery tuliwafata ndio hata kuonana na sisi hawakutaka inamaana huo mradi ya yeye unamhusu ndio mana kajiweka mwidho wa mwezi anchake
 
Walionishtaki ni manispaa chini ya kampuni ya hiyo ya kuzoa taka
 
Na inavyosemekna kwamba hii kampuni iliyoshinda tenda ya kukusanya taka ya moto nvestment inamilikiwa na viongozi wa mtaa kama afsa mtendaji na mwenyekiti wa serikali za mtaa
 
Sisi wafanya biashara wa eneo hili tukasema kua tunao uwezo wa kuzoa taka wakakataa
 
Owk kaka ila hawatoniweka ndani kwa faini na makorokoro mengine
 
Siku moja tuliwaambia watuonyeshe vigezo walivyotumia wakutonyesha vigezo vya uzoaji taka viwandani na hivyo viwanda wanatakiwa kulipa 30000
 
Sehemu yangu mm na wenzangu kwa maduka yote kwa siku ndoo ya taka hatujazi! Hivi fikiria mkuu biashara ya simu inazalisha taka kwa kiasi gani na yote ni maduka ya simu
 
Kule mbagala ukikutwa unachoma moto takataka unakamatwa maana unazuia mapato ya wazoa taka..
 
Back
Top Bottom