Nimepewa shikamoo na mwanamama umri kati ya miaka 38 na 45

Nimepewa shikamoo na mwanamama umri kati ya miaka 38 na 45

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Loo! Dunia inakwenda kasi wakuu,

Mwanamama kanitamkia kwa sauti, "Kaka shikamooo", watu wote niliokuwa nao karibu wakageuka kunitizama, wakapigwa na bumbuwazi, bila iyana nikaitikia, "Marhabaaa, ujambo!!?" akaitikia kwa kutikisa kichwa, akanitazama, kisha akaendelea na safari! [emoji23][emoji23]

Tuanze kwenye mwonekano, mimi ni kijana, umri 20 to 24 yrs, lakini mwonekano wa kitoto sana, sio mnene kusema alitumia kigezo cha unene, sio mgumu kusema labda angetumia kigezo cha sura, sijui mama wa watu kawaza nini!

Hatujawahi kutana mahali

Nahisi salamu yake imesababishwa na vitu viwili!

1. Mahali nilipokuwa nimesimama, nilisimama na madalali wa nafaka wanaoupiga mwingi, hawakosi laki mbili kwa siku! Huenda kajua na mimi ni mmoja wao!

2. Huenda ugumu wa maisha, mawazo mengi! Akajikuta anantupia salamu bila kujua!

Swali: Ni kwa nini atabasamu sasa?

Hii dunia ina mengi!
 
Mimi nahitaji uniunganishe na hao madalali wa Nafaka
Njoo inbox
 
Loo! Dunia inakwenda kasi wakuu,
Mwanamama kantamkia kwa sauti, "Kaka shikamooo", watu wote niliokuwa nao karibu wakageuka kunitizama, wakapigwa na bumbuwazi, bila iyana nikaitikia
Achana na pombe za kwenye vichupa vya plastic kama double kick na Don.

Tayari umeshachakaa amekuona kama 50 years old.

Kuna mwamba ni classmate wangu primary school miaka ya 80's huwa nikiwabiaga watu huyu tulikuwa class moja huwq wanakataa katakata kisa ni hizo double kick.

Kwq mfano tajiri Lowasa na Kikwete mkubwa ni Kikwete, ukimleta Magufuli hapo ndio dogo kabisa lakini alishachakaa tayari imagine huyo ni Rais na ana kila kitu.

Kuna yule Onyango wa Simba ana miaka 27 tu.
 
Ulivaa suti..
Hapana mkuu, nilivaa modo yangu nyeusi ya kitambaa, tshirt yangu ya maloon yenye kola, sandle zangu nyeupe, kibegi changu cha mkanda begani, miwani myeusi na kisimu changu mkononi! [emoji3][emoji3]
 
Achana na pombe za kwenye vichupa vya plastic kama double kick na Don.

Tayari umeshachakaa amekuona kama 50 years old...
Awap! Mimi sinywi pombe, wala sigara sivuti mkuu! Nashindwa kujaribu, maake kuna mwanababa somewhere akipita karibu na ghetoni lazima ayumbe adumbukie mtaroni, anapayuka kupita kiasi! ila asubuhi akiwa anakwenda kazini anakuwa mpole kama nini! Naona kama nikizibugia, nitakuwa zaidi yake!
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Loo! Dunia inakwenda kasi wakuu,

Mwanamama kanitamkia kwa sauti, "Kaka shikamooo", watu wote niliokuwa nao karibu wakageuka kunitizama, wakapigwa na bumbuwazi, bila iyana nikaitikia, "Marhabaaa, ujambo!!?" akaitikia kwa kutikisa kichwa, akanitazama, kisha akaendelea na safari! [emoji23][emoji23]

Tuanze kwenye mwonekano, mimi ni kijana, umri 20 to 24 yrs, lakini mwonekano wa kitoto sana, sio mnene kusema alitumia kigezo cha unene, sio mgumu kusema labda angetumia kigezo cha sura, sijui mama wa watu kawaza nini!

Hatujawahi kutana mahali

Nahisi salamu yake imesababishwa na vitu viwili!

1. Mahali nilipokuwa nimesimama, nilisimama na madalali wa nafaka wanaoupiga mwingi, hawakosi laki mbili kwa siku! Huenda kajua na mimi ni mmoja wao!

2. Huenda ugumu wa maisha, mawazo mengi! Akajikuta anantupia salamu bila kujua!

Swali: Ni kwa nini atabasamu sasa?

Hii dunia ina mengi!
Kuna dem unamendea humu!
unataka umvue kyup!
 
Back
Top Bottom