Mamzalendo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 1,670
- 558
pole sana nadhani ungempiga vibao na wewe kidogo ili akome tabia za kupiga wanaume wazima barabarani kha hana adabu kabisa hata ingekuwa kweli sio sawa kukupiga, anyway wanawake tunaweza kama vipi wanaume muanze na nyie kutafuta haki zenu, kama wewe umepigwa mme wake ana hali gani huko nyumbani?
vipi,ulitoa machozi? Maana vibao ni balaa.....
Hahahaaaa!! Pole Buji!sikumbuki, ninacho kumbuka ni maumivu na nyotanyota tu
Dah bujibuji umenichekesha.
pole sana mkuu kwa matatizo, ila ingekuwa ni vizuri huyo mwanamke umwombe ili utafune hata mara moja!!!
Muda huu nikiwa nangoja basi ili nirudi nyumbani kutoka kazini mara nikamuona mke wa jirani yangu akija huku akiwa amenuna na kukunja sura.
Alikuwa anatembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande nilioko.
Aliponifikia, akanikunja shati na kuanza kunipiga vibao, nikiwa katika hali ya mshangao, watu waliokuwepo kituoni wakamshika, ndipo alipoanza kuporomosha matusi "mwacheni nimshikishe adabu, anampeleka mume wangu kunywa pombe na kumtafutia wanawake".
Watu wakamkokota, na mi nikawa naondoka kiunyonge tena kwa aibu, nyuma nilisikia watu wakisema umemkomesha nguruwe akome.
Dah... Kumbe unaweza kusingiziwa hivihivi kwa makosa ambayo hujafanya.
Lakini tunaambiwa shukuruni kwa kila jambo

Mkuu huyo mama amekumaindi tu anatafuta upenyo wa kukuingia.