Nimepima UKIMWI naambiwa majibu yana utata nirudi baada ya mwezi vipi kuna usalama kweli?

Labda mashine zao tata, achana nao nenda kapime pengine
 
Majibu yenye utata ndio majibu gani hayo?

Tafuta kituo chochote cha ANGAZA kapime huko, utapokea majibu yako muda mfupi tu na ya uhakika.
 
Waganga wa kienyeji nd'o zao. Nenda angaza hawanaga longolongo. n mepimia bugado
 
Kupima VVU tunatumia vipimo vya aina mbili. Ya kwanza ni Determine na ya pili ni Unigold. Determine tunatumia kudetect uwepo wa vvu na ili kujihakikishia tunatumia na unigold as a confirmatory test. Ili kuonesha kwamba umeathirika vipimo vyote viwili lazima vitoe mistari miwili. Inapotokea kipimo kimoja yaani Determine ikatoa mistari miwili na unigold ikatoa mstari mmoja hayo ndio tunayosema majibu tata. Na kwa kawaida inatakiwa urudie kupima baada ya siku kumi na nne na sio mwezi.
 
ufafanuzi makini sana huu
 
Mhh! Sasa hiyo 'saikolojiko tocha' mtu unakua nayo mwezi mzima wanaifikiria? Mi naona heri upime na kwengine upate uhakika maana huo mwezi wa kusubiria utakua mgumu kwako sababu kucha utakuwa unawaza
 
Kupima VVU tunatumia vipimo vya aina mbili. Ya kwanza ni Determine na ya pili ni Unigold. Determine tunatumia kudetect uwepo wa vvu na ili kujihakikishia tunatumia na unigold as a confirmatory test. Ili kuonesha kwamba umeathirika vipimo vyote viwili lazima vitoe mistari miwili. Inapotokea kipimo kimoja yaani Determine ikatoa mistari miwili na unigold ikatoa mstari mmoja hayo ndio tunayosema majibu tata. Na kwa kawaida inatakiwa urudie kupima baada ya siku kumi na nne na sio mwezi.

siku hizi mmecha kutumia SD bioline 1/2
 
Hapo yawezekana mshauri nasaha aliona kwa dhati kabisa wewe utapokea majibu na kukubaliana nayo. Kwa hiyo amekupa nafasi ya kuanza kujikubali kabla ya kuambiwa kitu chochote.
 
Kuna mshkaji juzi kati kaenda kupima kaanza kuulizwa ameshagonga mademu wangapi,kabla hajajibu,akafungua mlango na kusepa hajarudi tena.
 
Kuna wakati SD bioline 1/2 ziliingizwa kwa wingi sana na zilipokuja kukaguliwa zikaonekana ni feki wakati tayari nyingine zilikuwa zimeshasambazwa kwenye baadhi ya mikoa. Hivyo serikali ikasitisha matumizi ya SD bioline 1/2 na kuanza kutumia Determine kama kipimo cha kuanzia.
 
Utata ni pale majibu mawili tofauti yanapotokea kwa mtu mmoja( Specimen moja)
au vipimio vilivyotumika vinaposhindwa kutonyesha kwamba vimepima ( Control )

Usiwe na Hofu wewe Rudi baada ya Muda uliopangiwa na utapata uhakika wa hali yako
 
Nenda kituo kingine ukapime kuliko kuishi kwa mashaka muda wote huo wa mwezi mzima.
 
Back
Top Bottom