Nimepita jengo la bunge nimeliangaliaaa, kisha nikajiuliza, waliomo humo wanatusaidia nini?

Humo zimejaa mbuzz, chawa, kunguni, fisi na nguruwe! Hakuna watu humo.
 
Safari hii tumepigwa na kitu kikali,hatuna wawakikishi pale. Wanaongelea mawaziri wawe na sehemu zao maalumu za kustarehe,mwingine anataka Dar tupandishiwe bei ya mafuta sh. 100 kwa lita,wengine wanataka idadi ya majimbo iongezeke. Hawa hawa ndiyo walipitisha tozo hadi wananchi tulipopiga mayowe ndiyo wanajitia kustuka kana Kwamba siyo waliyoipitisha. Lilaaniwe bunge hili kibogoyo na la wapenda starehe
 
Kwenye Idadai ya majimbo kuongezewa, ingepita kura kwa wananchi ili wapiga kura kuridhia huu ufisadi mwingine, la sivyo tunaongezewa mzigo mwingine usio na faida
 
Kama wamenyamaza na kurizia Wastaafu Waanze kulipwa Mafao Kwa Kikokotoo sitaki hata kuwasikia. Yaani nikijaliwa kuishi sitapiga Kura ya Kuchangia Kiongozi yeyote Nchi hii. Labda niwe naishi Jimbo atakalogombea Esta Bulaya. Nipigie Kura yeye tuuuuu. Wao miaka mitano wanakusanyiwa Bulungutu la 300milioni. Sisi 40 Years tunapewa 38milioni. Eti zinazobaki watulipe kidogo kidogo Kwa miaka 12 na Nusu. Ukifa Salio ni la Serikalini wala haliwahusu Wanao😭😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…