Nimepita leo Halmashauri ya Dodoma, watu ni wengi sana wenye bahasha za khaki

MshikjiFlaniHivii

Senior Member
Joined
Feb 12, 2020
Posts
117
Reaction score
339
Ndugu zangu, jana nilifanikiwa kufika halmashauri pale ya jiji la Dodoma kupeleka Barua yangu ya maombi ya ukusanyaji wa postcode, watu walikua wengi sana wenye bahasha za kaki. Vijana walikuwa wengi sana.

Muda huu pia nimetoka pale, nikaangalia yule anaepokea zile bahasha anazipa namba, namba imefika 203 mpaka naondoka pale😭😭 nafasi zilizotangazwa ni 100 na bado kesho ndio mwisho. Si watafika 1000. MUNGU ATUSAIDIA TUSIO NA CONNECTION 🙏🙏
 
Amina! Kama Mungu ameamua kukupa atakupa!

Au nenda kwa mkurugenzi wa manispaa unalia na kusaga meno

Mwambie Mimi ni masikini, Sina ajira pia Nina kifafa... Naomba unipe Nafasi kwa ajili ya Matatizo Yangu!

Hakikisha unatoa machozi kweli

Hiyo itakuwa connection Tosha kabisa
 
Hahah naongezea asisahau tu kutoa salamu ya kilugha cha mkurugenzi ndio kifuate kilio kikuu
 
Mbna idad ndogo hyo sana hyo ration inakuwa two in one 2:1 uwezekano wa kuitwa kufanya Kaz Ni mkubwa mno kwa idadi hyo
 
Kama una kifafa hiyo kazi utapewa kweli?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…