Nimeponea chupuchupu kulipia kundi kwenye mtoko

Nimeponea chupuchupu kulipia kundi kwenye mtoko

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Siku ya jana Jumapili nikiwa nimechill home ilikuwa ni mbaya na nzuri kwangu, Ilikuwa nzuri pale nilipopigiwa na "Mdaiwa Sugu" kwamba anataka kurusdisha pesa niliyomkopa january 400,000 taslimu na hivyo akatuma pamoja na ya kumvumilia akatuma 430,000, Nlifurahi sana na hapo ndipo nilipofanya uamuzi uliofanya siku yangu ya jana iwe mbaya, Nikapata wazo la kumtoa out g.f wangu hoteli moja ya matawi ya juu hapa Mbeya, Kwenye mahusiano yetu tumewekeana kwamba wiki hii akilipia outing mimi outing inayofata nalipia, So kwa vile wiki iliopita alilipia outing basi outing ya jana ilibidi nilipie.

Kitu cha kwanza nlimtumia 50,000 ili atoke mwake, then nikaweka bajeti ya 150,000 kwa ajili ya ,chakula vinywaji,chumba na mafuta ya gari. Imefika mida ya jioni saa kumi hivi nikaenda kutafuta hoteli iliotulia then nikamwambia aje, Nikiwa nasubiri nikaona sio mbaya nipooze koo kwa juisi baridi na baada ya dakika 10 akaniambia kafika so nikamuelekeza eneo nilipo.

Kufumba na kufumbua nikashudia kitu ambacho sikudhania kabisa, My girlfriend kaja na wezake watano, Nimemtoa g.f wangu mitoko kibao lakini ni mara moja tu aliwahi kumleta rafiki moja tu, Kimya kimya nikajisemea moyoni,"Mama yangu!!!, Nimekwisha", Sikuonesha usoni kwamba nimekasirika so nika smile kibish kibishi, Viti kwenye meza niliyopo vilikuwa viwili so ikabidi waiter atupeke sehem tuliyotosha watu 7, Treni likaanza kuchochea waiter akaanza kuleta menu list, Kimbembe kikaanza wote wakahitaji redbull mbilimbili, Hapo nikawazaga ule msemo "ukimpa panya glasi ya maziwa atataka na siagi", So nilichofanya nikamtumia rafiki yangu meseji anipigie simu ajifanye ni boss wangu kwamba ananihitaji, Nikamsave jina "Boss" NA alivyopigia simu nikajifabya nimekereka nikamwambia g.f. wangu aipokee yeye, so rafiki yangu akafanya kama nilivyomwambia so hapo ndipo nilipoponea chupu chupu nikawaaga nikalipia hela ya red bull tu na juisi yangu kwa 65,000 tu nikamwachia msimba g.f wangu nikasepa.

Kiukweli hii tabia ya kualika kundi kwa huu usawa ni mbaya sana na nikaona sina haja ya kulipiza kisasi kwa kuwaleta marafiki zangu outing ya wiki ijayo ambayo girl friend wangu atalipia bali nikamchana live kwamba kitu alichotaka kunifanya ni kibaya sana ambacho kingenitoboa wallet na asije kurudia tena kukifanya pindi nimtoapo out,
 
Siku ya jana Jumapili nikiwa nimechill home ilikuwa ni mbaya na nzuri kwangu, Ilikuwa nzuri pale nilipopigiwa na "Mdaiwa Sugu" kwamba anataka kurusdisha pesa niliyomkopa january 400,000 taslimu na hivyo akatuma pamoja na ya kumvumilia akatuma 430,000, Nlifurahi sana na hapo ndipo nilipofanya uamuzi uliofanya siku yangu ya jana iwe mbaya, Nikapata wazo la kumtoa out g.f wangu sehemu ambazo hatujazoea kwenda out,Nikaona ni vtema kwenda hoteli moja ya matawi ya juu hapa Mbeya.

Kitu cha kwanza nlimtumia 50,000 ili atoke mwake, then nikaweka bajeti ya 150,000 kwa ajili ya ,chakula vinywaji,chumba na mafuta ya gari. Imefika mida ya jioni saa kumi hivi nikaenda kutafuta hoteli iliotulia then nikamwambia aje, Nikiwa nasubiri nikaona sio mbaya nipooze koo kwa juisi baridi na baada ya dakika 10 akaniambia kafika so nikamuelekeza eneo nilipo.

Kufumba na kufumbua nikashudia kitu ambacho sikudhania kabisa, My girlfriend kaja na wezake watano, Nimemtoa g.f wangu mitoko kibao lakini ni mara moja tu aliwahi kumleta rafiki moja tu, Kimya kimya nikajisemea moyoni,"Mama yangu!!!, Nimekwisha", Sikuonesha usoni kwamba nimekasirika so nika smile kibish kibishi, Viti kwenye meza niliyopo vilikuwa viwili so ikabidi waiter atupeke sehem tuliyotosha watu 7, Treni likaanza kuchochea waiter akaanza kuleta menu list, Kimbembe kikaanza wote wakahitaji redbull mbilimbili, Hapo nikawazaga ule msemo "ukimpa panya glasi ya maziwa atataka na siagi", So nilichofanya nikamtumia rafiki yangu meseji anipigie simu ajifanye ni boss wangu kwamba ananihitaji, Nikamsave jina "Boss" NA alivyopigia simu nikajifabya nimekereka nikamwambia g.f. wangu aipokee yeye, so rafiki yangu akafanya kama nilivyomwambia so hapo ndipo nilipoponea chupu chupu nikawaaga nikalipia hela ya red bull tu na jusi yangu kwa 65,000 tu nikamwachia msimba g.f wangu nikasepa.

Kiukweli hii tabia ya kuwalika kundi kwa huu usawa ni mbaya sana na nikaona nimchane live girl friend wangu kwamba kitu alichotaka kunifanya ni kibaya sana na asije kurudia tena kukifanya pindi nimtoapo out,
Damu wa hivyo siyo gf MKUU anakuchuna tu.Mimi hata kwa dawa hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu hayo ndo malipo ya kuwekwa ptofile picture ...ɟʇʇ
 
Mkuu ulipoteza maxi tatu muhimu. Bahata ya kujihakikishia kuwa wewe ndie mume wake mtarajiwa, akaona awalete mashoga zake aje awatambulishe shem wao... Ulivyokula kona utakuwa umemfedhehesha sana.
 
Mkuu pongez sana..umeitosa committee, umetumia teknik ya kijanja sana

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Matumizi mabaya ya pesa unaingiza sh ngapi kwa mwezi?

Waliosema fainali uzeeni hawakukosea
 
Back
Top Bottom