Habari wakuu.
Nasikitika kusema nimepoteza Cheti Changu Cha Form 4. Cheti hiko kimepotea pamoja na vyeti vingine ambavyo nilimpa bibi yangu anitunzie kwa kipindi hiki ambacho bado naendelea na masomo mengine. Je,kuna uwezekano nikapata kingine nikifatilia pale NECTA?
Asante!

Dogo wala usiogope, vyeti vya necta vinatolewa kwa waliomaliza shule kuanzia mwaka 2008 vina picha na viko kwenye system ya necta ila kabla ya hapo ukipoyeza cheti wanakupa statement of result.
Unachotakiwa kufanya kama vilipotea na kuna uwezekano kwamba mtu mwngne aliokota na anaweza kutumia unatakiwa kutangaza gazeti la serikali kama daily news,habari leo na uhuru la ccm.
Kisha unachukua ikurasa wa tangazo lako kwenye gazeti unakaa nalo hadi miezi 3 kisha unawapelekea necta hapo unalipia 100000 ya cheti kipya baada ya miezi 3 wanakupa kipya.
Kama kilipotea na una uhakika hakikuweza kuokotwa na mtu kama kuungua au mafuriko au panya au mchwa hutatakiwa kutangaza gazetini, nenda kwa mwenyekiti wa mtaa wa bibi yako akupe barua ya utambulisho kwamba ni kweli kililiwa na panya uipeleke necta fasta kisha ulipie usubiri miezi 3 upewe kipya.
Tembelea web ya necta kuna form pale na maelezo jinsi ya kupata cheti kipya.
Vyeti vya zamani vilikua vinachapishwa na kiuta na sio necta kwa hiyo wanajidai hawana kumbukumbu maana havikua na picha na havikua digitlized ndio maana watu walivichakachua sana.
Nakutakia kila la heri mdogo wangu.